Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Innocent Bashungwa akiongea na Wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na Waandishi wa habari baada ya kutembelea ujenzi wa maabara ya shirika hilo.
Jengo la maabara ambalo lipo katika ujenzi ambalo litaweza kukamilka ndani ya mwezi mmoja kwa maagizo ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Innocent Bashungwa baada ya kutembelea Ujenzi huo leo.
************
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Innocent Bashungwa ameshangazwa na usimamizi wa ujenzi wa jengo la maabara lenye ghorofa nane linalojengwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutomalizika kwa wakati ambapo inasemekana ni uzembe wa mkandalasi anaehusika na ujenzi hivyo amemtaka akamilishe ujenzi huo ndani ya mwezi mmoja na kukabidhi.
Ameyasema hayo leo Mh.Bashungwa baada ya kufanya ziara katika ujenzi huo.
Akizungumza na Wanahabari pamoja na Wafanyakazi wa TBS, Mh.Bashugwa amesema kuwa amemtaka mkandalazi aweze kumalizia ujenzi huo ifikapo Septemba mosi ili baadhi ya vyumba viweze kutumika kwa shughuli za TBS.
“Kufika tarehe moja mwezi wa kumi jengo hili hasa hasa zile flow nne za mwanzo ambazo kwajili ya matumizi ya maabara zinaanza kufanya kazi na matarajio yangu kuona mtanzania akituma sample ikiwezekana ndani ya siku mmoja inafanyiwa kazi na mtanzania kupata matokeo”.Amesema Mh.Bashungwa.
Aidha Mh.Bashungwa amesema kuwa mkandalasi alielezwa kuwa ujenzi umekamilika kwa asilimia 95 hivyo akaamua kuja kujilidhisha ukamilifu wa ujenzi huo na kushangazwa na ujenzi unaondelea pamoja na maekezo aliyoambiwa na mkandalasi.
Changamoto iliyobaki ni upungufu wa wafanyakazi hivyo amesema kuwa atahakikisha ndani ya serikali kulifanyia kazi suala hilo na kupata wafanyakazi wa kutosha katika maabara hizo.
Naye Mkurugenzi wa TBS Bw.Yussuf Ngenya amesema kuwa atahakikisha anatekeleza yote aliyoyaeleza Waziri ili kuweza kutimiza malengo na kiu ya watanzania katika kufikia uchumi wa Viwanda.
Hata hivyo kwa upande wake Mkandalasi wa anaesimamia ujenzi huo, Bw.Kasimili Msobi amesema kuwa kuna baadhi ya vitu vinahitaji kukalimishwa ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati hivyo kwa maelekezo aliyotoa Waziri atahakikisha wanakamilisha ujenzi huo ndani ya muda ambao umetolewa na Waziri.