Na.Alex Sonna,Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba wameanza vyema baada ya kuichapa mabao 3-1 Timu ya JKT Tanzania Mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji hatari na Mfugaji bora wa msimu uliopita Meddie Kagere aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya kwanza akifunga bao kwa kumalizia pasi ya kiungo mshambuliaji aliyekuwa kwenye ubora wake Mzamiru Yassin.
Mara baada ya kupata baoa hilo Simba waliendelea kulishambulia lango la wapinzani kama nyuki wakiwa na hasira kutoka kwa UDO SONGO ambao waliwatoa katika hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hadi timu zinaenda mapumziko wenyeji walikuwa tayari wameruhusu bao moja kwa bila lililofungwa na Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda Meddie Kagere.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya kiufundi na kutafuta njia ya kupata ushindi kutokana na maelezo ya makocha wao.
Dakika ya 58 yule yule Meddie Kagere alirudi tena kwenye nyavu za JKT Tanzania amalizia pasi kutoka kwa Mzamiru Yassin na kuwanyanyua mashabiki wa Simba waliojitokeza uwanjani kushuhudia kandanda hiyo.
Akichukua nafasi ya Deo Kanda Mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli FC Miraji Athumani aliiandikia bao la tatu Simba kwa kichwa mara baada ya kupokea pasi kutoka kwa Meddie Kagere.
Akitokea benchi Mshambuliaji Edward Songo aliipatia timu yake bao la kufutia machozi mnamo dakika ya 87 akiachia shuti kali lililomshinda mlinda Mlango wa Simba Aish Manula na kumuacha akilala bila mafanikio.
Hadi dakika 90 za Mwamzi Heri Sasii akipuliza filimbi ya mwisho Simba wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kujinyakulia alama zote tatu.