Wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wanawake Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Amina Tindwa wa kwanza kushoto alibeba katoni ya sabuni wakiwa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo kilichopo Sanangula Manispaa ya Songea wakitoa msada wenye thamani ya shilingi 425,000.
************************
WANAWAKE kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 425,000 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo kilichopo mjini Songea.
Wanawake hao wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuelekea siku ya wanwake Duniani ambayo kilele chake ni Machi 8 mwaka huu.
Akizungumza kabla ya kutoa msaada huo, Mwenyekiti wa Wanawake katika Ofisi hiyo Amina Tindwa amesema katika kuadhimisha wiki ya Wanawake Duniani wanatembelea vituo mbalimbali vya watu wenye uhitaji na wanaoishi kwenye mazingira magumuj kwa kuwa mwanamke ni mlezi katika familia.
“Msaada ambao tumeutoa katika kituo hiki ni mbolea pamoja na bidhaa zingine ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi 425,000’’,alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo hicho Sista Benigina Kapinga amesema kituo hicho kina watoto 24 ambao mmoja yupo chuo na wengine wanasoma shule za Sekondari na shule za msingi.
Sista Kapinga amewashukuru wanawake hao kwa moyo wa upendo ,hata hivyo ameiomba serikali kusajiliwa kituo hicho ili kitambulike na waweze kupata misaada mbalimbali.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Exerveria Mlimila amemshauri Mkuu wa kituo hicho kufanya jitihada ya kusajili kituo hicho ili kitambulike na kuweza kupata misaada mara kwa mara hivyo kukidhi mahitaji ya watoto hao.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Marchi 3,2022.