**************
NJOMBE
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania[JWT] Amesema Kuwa Endapo Hakutafanyika Marekebisho ya Sheria za Kodi Pamoja na Kuweka Sawa Tozo za Kodi Bandarini Basi Wafanyabiashara Wote Huenda Watafungwa Kwa Kutoa Rushwa Inayopingwa Vikali na Serikali ya Awamu ya Tano.
Katika Mkutano Mkubwa wa Wafanyabiashara Walioiwakilisha Mikoa Takribani Kumi Ukiwemo Mkoa wa Kibiashara Mafinga ambao Wamekutana Mjini Makambako Mkoani Njombe Baadhi ya Wafanyabiashara Hao Akiwemo Kolar Benitho,Sifael Msigala na Aman Mahela Wamesema Kuwa Suala la Kutozwa Faini Kwa Kile Kinachoelezwa ni Kutolipa Kodi Kwa Kipindi Cha Miaka Kadhaa Wakati wa Mahesabu ya TRA Kwa Mfanyabiashara Kumekuwa Kukisababisha Kuingia Kwenye Mazungumzo na Mtozo Kodi Ili Kutoa Rushwa Kwa Kuwa Wanashindwa Kutunza Kumbukumbu.
Akitolea Ufafanuzi wa Kero Mbalimbali za Wafanyabishara Hao Kamishna wa Kodi Tanzania Edwin Mhede Amesema Hakuna Namna Nyingine Katika Ukusanyaji Kodi Kwa Wafanyabiashara Wasiotunza Kumbukumbu za Biashara Yao zaidi ya Kujifunza kwani suala la kodi lipo kwa Mujibu wa Sheria na Kwamba Suala la Rushwa Atalipinga Kwa Nguvu Zote Kwa Pande Zote.
Maelekezo ya Kamishna Huyo Yamemfanya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Abdalah Mwinyi Kutaka Kufanyike Marekebisho ya Sheria ya Kodi Pamoja na Kuwekwa Sawa Bandarini Ambako Kumeonekana Kuwa na Tozo Kubwa za Kodi ya Mizigo Vinginevyo Rushwa Haitokoma Kwa Wafanyabiashara Hao Nchini.
Baada ya kusikiliza kero hizo , kisha waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa anatoa kauli ya serikali ambapo anasema tayari serikali imefuta kodi 54 pamoja na kupunguza mamlaka za kutoa leseni za biashara huku pia akieleza hatua iliyofikiwa kuhusu kuandaa blue print itakayokuwa muongozo katika sekta ya biashara.