Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) Onesmo Olengurumwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakitoa ushauri wao kama Watetezi kuhusu Mgogoro wa Ardhi Wilayani Ngorongoro.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Mashirika ya Wafugaji-Pingos Forum bw.Edward Porokwa akieleza changamoto ambayo Wananchi wa Ngorongoro wanaokumbana nayo.
Wakili Haki Ardhi Joseph Chombola akizungumza mbele ya wanahabari akieleza kuhusu Mgogoro wa Ardhi Wilayani Ngorongoro.
Mratibu wa Jukwaa la Ardhi Tanzania Bernard Baha akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akitoa ushauri kuhusu Mgogoro wa Ardhi Wilayani Ngorongoro
………………………..
NA MUSSA KHALID
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini umemuomba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunguano wa Tanzania Kassim Majaliwa kuwapa nafasi wadau huru wakiwemo Wananchi wa Ngorongoro,watetezi wa Haki na wadau wengine kushiriki Katika kutoa elimu Kwa wabunge kuhusu hali ya Wilaya ya Ngorongoro.
Akizungumza na wanahabi Leo jijini Dar es salaam Mtaribu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRDC) Onesmo Olengurumwa amesema ni vyema Waziri Mkuu akatoa fursa kwa wananchi na wadau hao kwani bila kufanya hivyo kunaweza kuchochea taarifa za upande mmoja wa makundi mbalimbali yanayovutana kuhusu Ngorongoro.
Aidha Olengurumwa ameikumbusha serikali kuzingatia kwamba Mwaka 1958 Hifadhi ya Ngorongoro ilipoanzishwa ilikuwa na malengo makuu matatu ikiwa ni pamoja na Uhifadhi,kulinda maslahi ya wenyeji waliondolewa Serengeti Kwa mkataba na wakoloni,lakini pia na Utalii.
“Tunaiomba serikali iunde tume huru itakayowahusisha wafugaji wenyeji wa Ngorongoro,Wataalamu wa uhifadhi,watetetezi wa haki za Binadamu,wadau wa utalii,wataalamu wa mifugo Ili ufanyike utafiti jumuishi kuhusu hoja zinazobishaniwa na baadae kuja na mapendekezo yatakayozingatia ulinzi wa Hifadhi pampja na haki za Jamii ya Ngorongoro.”amesema Olengurumwa
Aidha Mtaribu Huyo wa THRDC ameiomba serikali kutambua kuwa kitendo cha kuwaisha watu wa Ngorongoro na Loliondo kunaweza kusababisha Madhara Kwa Jamii Hizo ikiwemo kuwakosesha Amani, uhuru na Maendeleo Katika vijii vyao.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Mtandao wa Mashirika ya wafugaji- Pingos Forum Edward Poroka amesema wamesikitishwa na taarifa za baadhi ya waandishi wa habari ambao hivi karibuni walikuwa wakutafuta nafasi ya kuwasikiliza Wananchi kusumbuliwa wakati wanafanya Kazi zao huko Ngorongoro.
“Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kumuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kukutana na Wananchi wa Ngorongoro na Loliondo Ili kuwasikiliza na kutatua changamoto zilizopo kwa Pamoja,Pia tunampongeza Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Akson kwa kuiagiza serikali kutafuta Suluhu ya kudumu ya mgogoro huo wa ardhi.”amesema Poroka
Poroka ameishauri serikali kukaa na Wananchi kujadili juu ya mgogoro huo unaoendelea ili kuondoa upotoshaji unaoenezwa na baadhi ya watu wenye maslahi binafsi na Taasisi nyingine Ili kupata mwafaka wa Pamoja.
Naye Wakili wa Haki Ardhi Joseph Chombola ametumia fursa hiyo kusema kuwa changamoto za Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro zimekuwa zaidi kutokana na ugumu wa kutenda Kazi Katika maeneo hayo kwa Watetezi wa Haki za Binadamu, waandishi na wanasheria waliotayari kusaidia Wananchi akieleza miaka ya nyuma baadhi walaiwahi kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kughushi Pamoja na makosa ya uchochezi.