Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama,akizungumza na wadau wakati wa warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma
Muwakilishi kutoka shirika la FAO Bw.Fred Kafeo,akisoma taarifa wakati wa warsha uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uvuvi wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Emmanuel Bulayi,akiongea na wadau wakati wa warsha uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua warsha wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Kaimu Meneja Mkuu Shirika la Uvuvi Tanzania TAFICO Bi. Esther Mulyila wakati wa warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kuzindua warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
…………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imesema iko katika michakato wa kulifufua Shirika la Uvuvi la Taifa (TAFICO) ambalo litajiwekeza katika uvuvi wa samaki kwenye ukanda wa bahari kuu.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama wakati wa warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi.
Amesema malengo ya serikali ya kuifufua TAFICO inatarajia kuwa na tija kubwa kutokana na mipango iliyopo katika kuiendeleza sekta hiyo.
“Mipango yetu ni kuhakikisha hii sekta unakuwa na serikali inafanya michakato ya kuifufua TAFICO na Mambo mazuri yanakuja” amesema Dkt Tamatama.
Amebainisha mpango mpya kabambe wa uvuvi unaelekeza sekta kusimamia, kuhifadhi na kulinda ili sekta hiyo itoe mchango mkubwa kwenye lishe kwa mtu moja moja na usalama wa chakula na kuelekeza sekta ili itoe mchango kwa uchumi,
Amesema mpango uliozinduliwa mwaka 2002, ulimalizika mwaka 2015 na mafanikio ya mpango ule upande wa pwani kuna maboresho makubwa ya uvuvi wakati wa mradi uliojenga mialo nyingi na kukopesha zana za kuvulia vikundi mbalimbali vya uvuvi, pia kuna mradi mwingine wa benki ya dunia.
Kwa upande wake kaimu Meneja Mkuu wa TAFICO, Ester Mulyila, amesema Shirika hilo linatazamiwa kufufuliwa hivi karibuni na menejimenti ya kufufua shirika hilo waliteuliwa kuanza taratibu za kufufua shirika.
Amesema TAFICO ilianzishwa 1974 wakati wa serikali ya awamu ya kwanza, ili kuendeleza shughuli za uvuvi makao makuu Dar es salaam na ilifanya kazi Pwani yote ya Tanzania kuanzia Tanga,mpaka Mtwara ziwa Victoria.
Lingine ni Tanganyika Nyasa kubwa mpaka mwaka 1996 ikijihusisha na uvuvi hasa wa kambamiti ilikuwa na meli, viwanda vya kutengeneza mashua za mbao na chuma, mitambo ya kuzalisha barafu, maghara ya kuhufadhia samaki.
Amebainisha mwaka 2008 wizara ya maliasili na utalii ilikuwa na dhamana ya uvuvi iliuza vitu vinavyohamishika kwa taratibu za serikali msajili wa hazina, lakini mali zisizohamishika zilibaki viwanja na majengo vilibaki kwa matumizi ya serikali.
Serikali ya awamu hii.imeongeza nguvu ya kutaka kufufua shirika waraka wa baraza la mawaziri imeelekeza shirika hilo kufufuliwa, lengo kuwezesha serikali kunufaika na raslimaliza zake za uvuvi hasa zilipo uchumi wa bahari kuu una ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 223,000 ikiwa ni sawa na robo ya Tanzania nchi kavu.