Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe akifungua mkutano wa 53 wa utabiri wa msimu wa vuli kwa nchi 11 za pembe ya Afrika unaofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam.
…………………………………………….
WATAALAM wa sayansi ya Hali ya hewa wameshauriwa kuzingatia njia za asili za kutambua hali ya hewa ijayo na kuziboresha.
Ushauri huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe alipofungua mkutano wa 53 wa utabiri wa msimu wa vuli kwa nchi 11 za pembe ya Afrika.
Mhandisi Kamwelwe alisema ni vema poaa kutumia pia njia za asili za kutabiri hali ya kuliko kuachana nazo kabisa huku akisisitiza kwamba njia hizo zinaweza kuboreshwa.
“Hata wakati wa kubadili sheria kutoka kwenye Agency kwenda kwenye Authority tulipata ushauri kwamba hata kakakuona tunaweza kumtumia kuandaa utabiri,” alisisitiza Waziri Kamwelwe.
Waziri huyo aliwataka washiriki 200 wa mkutano huo watatoka na maazimio yatakayochangia upatikanaji wa taarifa sahihi zaidi za hali ya hewa ili kuwasaidia watumiaji wa taarifa hizo kwenye shughuli zao za maendeleo kwa nchi shiriki.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi alisema wataalam hao pamoja na kujadili msimu ujao wa mvua za vuli watatoka na utabiri wa nchi wanachama kwa maendeleo ya nchi zao.
“Hii ni mikutano inayofanya mara kwa mara kabla ya kuandaa taarifa ya msimu kwenye nchi zetu huwa tunakutana na kutoa utabiri wa ukanda wetu huu.
“…Naamini mkutano huu utakuwa na matokeo chanya hivyo basi watumiaji wa taarifa zetu waendelee kusubiri,” alisema Dk. Kijazi huku akifurahia Tanzania kupewa heshma ya kuandaa mkutano huo muhimu Afrika.
Kuhusu mvua zinazoendelea, mkurugenzi huyo alisema zipo nje ya msimu huku akibainisha keamva ni mabadiliko yaliyosababisha kupungua kwa mkandamizo wa hewa baharini jambo linalosababisha unyevu kwenye anga.
“Sio mvua kubwa na hazitachukua muda mrefu, hizi zipo hasa ukanda wa Pwani na mikoa inayozunguka Ziwa Victoria… Wananchi wasihofu,” alisema Dk. Kijazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TMA, Burhani Nyanzi alisema mkutano huo unalenga kuwasaidia watu wote wanaofanya shughuli zao wakitegemea hali ya hewa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.
Picha mbalimbali zikionesha washiriki wa mkutano huo kutoka nchi 11 za pembe ya Afrika.