Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Achiles Bufure (aliyevaa koti juesi la suti kushoto), Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa Augustino Makame (wa Pili Kushoto),Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Tanzania Cynthia Henjewele (Kulia),Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Elia Mjata (wa pili Kulia) wakiwa Pamoja wakiwa mbele ya wadau mbalimbali Kwa ajili ya kujadili namna ya kuboresha Tamasha la Museum Art’s Explosio Katika hafla ambayo imefanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam
Cultural attachee kutoka Ubalozi wa Uturuki akichangia mjadala
Watanzania wametakiwa kupenda kushiriki katika matukio yanayotangaza kazi za wasanii wa ndani likiwemo Tamasha la Museum Arts Explosion linalotarajiwa kufanyika Makumbusho ya Taifa kila wiki ya mwisho wa mwezi.
Akizungumza leo jijini Dar es leo jijini Dar es salaam Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa katika Mkutano wa wadau wa sanaa katika Program ya Museum Art’s Explosion Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Achiles Bufure amesema lengo lao ni kurithisha watanzania urithi uliopo Nchini kupitia vipaji vyao.
Aidha Bufure amesema progamu hiyo ya sanaa na wasanii ilianza tangu Mwaka 2016 ikiwalenga kuwakaribisha wasanii wanaofanya kazi za ufundi wa mkono na wa majukwaani kwenda kuonyesha vipaji vyao.
“Kama tunavyojua hapa katikati tumekumbana na changamoto ya maradhi ya UVIKO-19 katika kufanya maandalizi lakini pia za wadau wenyewe kuwa na muamko wa kujitokeza hivyo kwa leo kabla ya kuanza Tamasha la Mwaka huu tumeona tukutane Ili kujadili kuhusu faida na namna gani tutafanikisha liweze kuwa bora zaidi na kuondokana na changamoto”
Bufure amesema kuwa lengo lao ni kutaka watanzania watambue na kuelewa sanaa zao ziwe za ubunifu,za mikono pamoja na za jukwaani Ili waweze kuwa wazalendo wa tamaduni zao kwani pia Sanaa ni kazi kama zilivyokazi kazi ngingine.
Kwa upande wake Afisa Sanaa Mwandamizi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa Augustino Makame amesema Baraza hilo linajivinia kupitia program hiyo kwani wasanii na vijana mbalimbali wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika maonyesho lakini pia inawasaidi kujiongezea masoko.
Naye Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Tanzania Cynthia Henjewele amesema malengo ya uwepo Tamasha hilo litasaidia kumkomboa msanii kwenda kupata ajira kutokana na kujulikana zaidi na kujitangaza na hivyo kuonekana na wadau mbalimbali watakaojitokeza kutoka Nje na ndani ya Nchi.
“Hivyo natoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonyesho hayo Ili waweze kuona vijana wakitanzania wakionyesha vipaji vyao”amesema Henjewel
Kuhusu ushiriki wa wasanii wa filamu,Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Elia Mjata amesema watahakikisha wanapopata nafasi wanafanya vizuri na kuongeza motisha ya watu kujitokeza kwa wingi katika matamasha hayo hivyo kuongeza muamko Mkubwa kutokana na ubunifu watakaoufanya.