Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita wa jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Alfred Kapinga ( Wakwanza kushoto ) Akimvisha Mkanda wa Ubingwa Afrika mashariki na kati bondia Tonny Rashid aliyeshinda baada ya Kumpiga Haidary Mchanjo katika pambano lililofanyika Club 361 Mwenge Jijini Dar Es salaam.
Mabondia wa kulipwa Nassibu Ramadhani na Issa Nampepece wakitifuana wakati wa Mchuano wa Ubingwa Afrika mashariki na kati katika Ukumbi wa 361 Mwenge Bondia Nassib Ramadhani aliibuka Mshindi.
Bondia haidary Mchanjo akimtupia konde Bondia Mwenzie Tonny Rashidi katika Mpambano wa kuwania ubingwa Afrika mashariki na kati Tonny Rashidi aliibuka na ushindi kaptika mpambano huo uliofanyika Club 361 Mwenge.
***************
Katika Mpambano wa Kwanza Nasibu Ramdhani alishinda kwa Pointi 99/91 jaji wa pili 100/90 jaji wa Tatu 99/91 baada ya Mchuano Mkali wa Vuta Nikuvute uliowapelekea kumaliza Raundi zote 10 za Mchezo huku mashabiki wakishuhudia Ngumi za Kuvutia za kila mmoja kumuwinda mwenzie.
Mara baada ya Mpambano huo Nassibu Ramadhani alisema mpinzani wake Issa Nampepeche ni Bondia Mzuri na alitumia Mbinu za kutoka ndio ambazo zilimfanikisha kumaliza Mpambano huo kwa Rundi zote 10.
Naye Bondia Issa Nampepeche alisema Mpinzani wake alikuwa Mzuri zaidi hivyo anaenda kujipanga upya baada ya kupoteza mchezo huu na anaimani kufanya Vizuri katika Michezo mingine inayofuata.
Katika Mpambano mwingine Bondia Tonny Rashidi aliibuka na Ushindi kwa pointi toka kwa Majaji Wote Watatu ambapo walimpa 97 kwa 93 jaji wa pili 98/92 na Jaji wa Tatu 99/91 Dhidi ya Haidary Mchanjo baada ya kumalizika kwa raundi 10 katika pambano ambalo lilikuwa na hamasa kubwa ya kutakiwa kupatikana kwa mbabe baada ya pambano la Awali kumalizika kwa sare.
Naye Bondia wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Selemani Kidunda alidhihirisha Ubabe wake baada ya kushinda kwa KO katika Raundi ya Kwanza ya mchezo Sekunde ya 45 baada ya kumtwisha Konde bondia Nassoro Hussein.
Mchezo mwengine
Katika Ngumi za wazi Mabondia wa JWTZ waliokuwa wakijipima Uwezo kwa ajili ya kujiandaa na Mashindano ya Dunia ya Majeshi Nchini China Bondia George Costatino alimshinda Bondia Osama Araba wa Jeshi la Anga ,Ismali Galiatano alimshinda kelvin kipinge, Fabian Gaudence alishinda kwa Pointi Dhidi ya Athanas Ndigaya.
Katika mchezo mwingine Alex Michael alishinda kwa KO Raundi ya tatu Dakika ya pili dhidi ya Mussa Ally na Kassim Mbundwike naye alishinda kwa KO raundi ya kwanza Sekunde ya 30 dhidi ya Julius Nickson wa Jeshi la Anga na Bondia Mwanmke Irene Kimaro alimtwanga Stumai Muki kwa Pointi.