Meneja huduma wa Kampuni ya Pan African Energy Tanzania (PAET) Injinia Peter Sororo akitoa maelezo kwa Bw. Martin Mwambene Msemaji wa TANESCO aliyeongozana na baadhi ya maofisa wa TANESCO Kitengo cha Mawasiliano na waandishi wa habari kuhusu Genereta tatu zinazofungwa katika mitambo ya kuchakata gesi ya Songas Songosongo wilayani Kilwa mkoani Lindi katika maboresho ya visima vya kuzalishia gesi asilia.
(PICHA JOHN BUKUKU-SONGOSONGO-KILWA)
Meneja huduma wa Kampuni ya Pan African Energy Tanzania (PAET) Injinia Peter Sororo akitoa maelezo kwa baadhi ya maofisa wa TANESCO Kitengo cha Mawasiliano na waandishi wa habari kuhusu Genereta tatu zinazofungwa katika mitambo ya kuchakata gesi ya Songas Songosongo wilayani Kilwa mkoani Lindi katika maboresho ya visima vya kuzalishia gesi asilia.
Baadhi ya mitambo mipya inayofungwa katika visima hicho ili kuongeza uzalishaji.
Hizi ni Genereta kubwa tatu mpya zinazofungwa ambazo zitaendesha mitambo ya kuchakata gesii na kuisukuma kwenda kwa wateja nchini.
…………………………………………….
Meneja huduma wa Kampuni ya Pan African Energy Tanzania (PAET) Injinia Peter Sororo amesema maboresho katika visima vya kuzalishia gesi asilia (Songosongo) yataambatana na faida kubwa ikiwemo ya kuongezeka kwa kiwango cha gesi ikizingatiwa kuwa kadri ya muda unavyokwenda nguvu ya gesi kujisukuma kwenda kwa wateja inapungua.
Ametanabaisha kuwa lengo la maboresho hayo ambayo hadi leo yamefikia siku ya tatu lililikua kuongeza kiwango cha uzalishaji wa gesi ili kufikisha kwa wateja kiwango kinachohitajika huku ikitarajia kuanza kuzalisha kiasi cha futi Milioni 90 kwa siku ambacho hakikuwai kuzalishwa hapo awali.
Injinia Peter Sororo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea visima hivyo na kujonea shughuli za maboresho ya visima hivyo ukiwemo ufungaji wa mitambo mipya kazi ambayo inaendelea vizuri.
Ameongeza kuwa kufanyika kwa maboresho hayo kutaongeza ujazo wa uzalishaji gesi kwa kiasi cha futi milioni ishirini na tano kwa siku na hivyo kufanya kiasi cha gesi kitakachozalishwa kwa siku kufikia milioni 105 ikijumlishwa na kiasi cha futi milioni 80 zilizokuwa zikizalishwa kwa siku kabla ya kuunga visima viwili.
“Mpango tulioufanya tuliamua kupeleka visima vyetu viwili kwa GASCO hatua iliyowawezesha kuongeza uzalishaji wa gesi kwa kipindi hiki cha siku kumi, kutoka wastani wa futi Milioni 30 hadi 35 hadi milioni 90,”Amesema Injinia Peter Sororo.
Amefafanua kuwa kazi ya maboresho kwa sasa imefikia asilimia 30 huku uongozi wa kampuni ya Pan African Energy Tanzania(PAET) inayohusika na mradi huo ikiahidi kumaliza kazi hiyo ndani au kabla ya siku kumi zilizokusudiwa.
Hatua hiyo kama itatekelezeka kuna uwekezano tatizo la upungufu wa umeme lililotajwa na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kuwa lingechukua muda wa siku kumi likamalizwa mapema tofauti ya muda uliokusudiwa.
Ameongeza kuwa Mradi huo umekuja ili kuhakikisha muendelezo wa uzalishaji wa gesi unaendelea..lakini pia kuhakikisha tunafikisha gesi kwa wateja wetu kwa mgandamizo unaohitajika, ijulikane kwamba kila unapozalisha gesi kiwango kinapungua hivyo hakukuwa na namna nyingine Zaidi ya kuwa na hizo siku kumi za kufanya maboresho hayo ili kuongeza uzalishaji wa gesi.