Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na Meneja RUWASA Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Christine Kessy akikagua tenki la maji la Mradi wa Maji wa King’ori.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro akikagua Mradi wa Maji wa Makilenga na kusikiliza kero za wanakijiji Oldonyong’iro.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akizungumza na wakazi wa Kijiji cha King’ori, wilayani Arumeru katika Mkoa wa Arusha.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongoza kikao kilichohusisha viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru, wajumbe ya Bodi ya Mradi wa Maji wa Makilenga na wananchi.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akionyeshwa nadharia ya utekelezaji wa mradi wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kabla ya kuukagua.
…………….
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza wajumbe wa Bodi ya Makilenga inayosimamia Mradi wa Maji wa Makilenga, wilayani Arumeru, mkoani Arusha akiwemo Mwenyekiti na Mhasibu wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya ubadhirifu wa fedha.
Mhe. Aweso amewachukulia hatua wajumbe hao kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na kusababisha wakazi wa Kijiji cha
Oldonyong’iro kukosa huduma ya maji.
Ameelekeza timu kutoka Wizara ya Maji na Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru ifanye uchunguzi kwenye Mradi wa Maji wa Makilenga na kumpa ripoti haraka.
Wakati huo Mamlaka ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru wasimamie mradi kwa kipindi chote cha mpito, mpaka viongozi wengine watakapopatikana.
Aidha, Naibu Waziri Aweso amekagua ujenzi wa mradi wa majsafi na salama wenye lengo la kuimarisha huduma endelevu ya maji na usafi wa mazingira kwa wananchi 50,000 kupitia teknolojia bunifu katika maeneo ya Lengijave, Olkokola, Ngaramtoni, Ekenywa na Seuri yaliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Pamoja na vijiji vya Lemanyata, Lenjani, Ilkerundeti, Ilikuroti na Lemanda kwa siku zijazo.
Mhe. Aweso amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Assess kumaliza mradi huo uliofikia asilimia 97 ya utekelezaji haraka.
Mkandarasi huyo ametoa ahadi ya kukamilisha mradi huo ifikapo Septemba 1, 2019 na wananchi wataanza kupata maji.