RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar, wakati wa kuwasilisha Utekelezaji Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo,23-8-2019.(Picha na Ikulu).
WATENDAJI mbalimbali wa Idara za Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakati ikiwasilishwa Ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yao, Mkutano huo ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe,. Balozi Ali Abeid Karume, akiwasilisha ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, wakati wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, kulia Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Lulu Msham Abdalla na Mshauri wa Rais Sanaa na Utamaduni Mhe. Chimbeni Kheri.(Picha na Ikulu).
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Ndg Amour Hamil Bakari, akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, kushoto Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Bi. Saum Ali Said na Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg. Joseph Kilangi.(Picha na Ikulu)
MSHAURI wa Rais Masuala ya Sanaa na Utamaduni Mhe Chimbe Kheri akizungumza wakati wa mkutano na Uongozi wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar, kuzungumzia Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo uliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)