Balozi wa Tanzania Nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akizungumza katika
Ugeni wa Wataalam wa Mtandao wa BAIDU (hawapo pichani) katika hafla fupi kuhusu
namna ya uzalishwaji wa Film ya vivutio vya Tanzania iliyofanyika mapema Jijini Dar
es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya TTB Richard Rugimbana akizungmza na wageni kutoka
matandao wa BAIDU (hawapo pichani), katika hafla fupi kuhusu uzalishwaji wa Film ya
vivutio vya Tanzania iliyofanyika mapema Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania Nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki(wa tatu kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Mtandao wa BAIDU katika hafla fupi
kuhusu namna ya uzalishwaji wa Film ya vivutio vya Tanzania iliyofanyika mapema
Jijini Dar es Salaam, wataalam hao wako nchini wa siku 11 kutembelea vivutio na
badaye kuzalisha Film na kupiga picha.
Balozi wa Tanzania Nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki(wa tatu kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Mtandao wa BAIDU katika hafla fupi
kuhusu namna ya uzalishwaji wa Film ya vivutio vya Tanzania iliyofanyika mapema
Jijini Dar es Salaam, wataalam hao wako nchini wa siku 11 kutembelea vivutio na
badaye kuzalisha Film na kupiga picha.
*****************
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
22-08-2019
Kampuni za Beijing Pseacher Business na Baidu toka nchini China wamejikita katika tafiti za hatua za mwisho ili kutengeneza picha mnato na mjongeo(Film)
zitakazowekwa kwenye mtandao wao wenye wafuasi takribani 700, lengo likiwa
kuinua utalii nchini.
Balozi wa Tanzania Nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki, katika mahojiano mwishoni mwa wiki, Jijini Dar es salaam, amesema Tanzania ni nchi ya kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki yenye vivutio vingi vya kiutalii, na kwamba ujio wa wageni wanaoongezeka kutoka China ni neema kwa sekta ya utalii.
“Kampuni hizi ni mawakili, yaani Beijing Pseacher Business na Baidu wameanzisha
programu maalum ya kutangaza vivutio vya utalii duniani na wameamua nchi ya
kwanza watakayoanza nayo katika kazi hii ni Tanzania”, Alisema Balozi Kairuki
ambapo tayari wameanza hatua za kuandaa andiko (script).
Hata hivyo Balozi Kairuki alisema kuwa Tanzania imechaguliwa kuwa ya kwanza
kwenye mradi huo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo binadamu wa kwanza kuwepo hapa Tanzania, mbuga kubwa za wanyama na maeneo mazuri ya kupumzikia kama vile fukwe.
Aliongeza kuwa lengo la Bodi ya Utalii, TTB kuhusiana na zoezi hili kutoka China ni
kuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengi kutoka China kuja kutembelea
Tanzania na pande hizi mbili zinatambua vivutio vitakavyochukuliwa kwenye mradi
huo wa picha na itakuwa fursa kubwa kwa Tanzania.
“Hii ni fursa kubwa kwetu kujitangaza katika soko la utalii la China na kufahamika
kwa wachina wengi na hatimaye idadi ya watalii kutoka china kuongezeka, tulikuwa tukipata watalii elfu 34 kwa mwaka, lakini program hii inalenga kufikisha watalii elfu 50, ifikapo mwaka 2020 na laki moja mwaka 2025”, Alisema Balozi Kairuki.
Aidha Balozi Kairuki alisema kuwa katika kutekeleza hilo Serikali imejipanga
kikamilifu huku Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) likiwa katika hatua za mwisho
kuanzisha safari za moja kwa moja kwenda China.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Utalii,Richard Rugimbana amesema kuwa tukio la uzalishaji wa filamu hiyo kubwa ya vivutio vya utalii Tanzania na baadaye
kufanikiwa kuiweka kwenye mtandao huo mkubwa litakuwa ni tukio la kihistoria kwa Tanzania na sekta ya utalii kwa ujumla.
“Tukio la leo (alhamisi) ni tukio la kihitoria kwa maana ya kwamba kampuni za
kimataifa za Beijing Pseacher Business na Baidu wameamua kuichagua Tanzania kwa Afrika nzima na kuitangaza, kwani ni nchi pekee ambayo wataweza kupata vitu vizuri vya utalii”, Alisema Richard Rugimbana
Richard alisema kuwa mtandao huo wa Baidu una zaidi ya wafuasi milioni 700 kwa hiyo itakuwa ni rahisi kwa vivutio vya Tanzania kuwavuta watalii wengi kwenye soko la utalii wa Tanzania kama uwekezaji.