Mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa Dr. Abel Nyamahanga,Meneja wa TARURA Wilaya ya Iringa Barnaba Selemani Jabir na mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakiwa wanapita kwenye daraja lililosimamiwa na TARURA wilaya ya Iringa
Meneja wa TARURA Wilaya ya Iringa Barnaba Selemani Jabir akiwa na mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya ya Iringa Makala Mapesah na mwenyekiti wa wazazi CCM mkoa
**************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA cha mapinduzi Mkoa wa Iringa kimesema wakala wa barabara TARURA Wilayani Iringa imetekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali ya kuharakisha maendeleo kwa wananchi kwa kufanikiwa kutekeleza miradi yao kwa wakati
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya Siasa ya chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa (CCM) ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, Mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa Dr. Abel Nyamahanga akiongoza katika ziara ya amesema wameridhishwa na TARURA hasa kwa kufanikisha ujenzi wa daraja la Ifunda.
Dr. Nyamahanga alisema kuwa kamati ya siasa ya mkoa wa Iringa inapongeza na kueleza kuridhishwa na namna ambavyo TARURA wanavyotekeleza miradi yao huku akisisitiza kuwa mradi wa ujenzi wa barabara Na daraja la Ifunda Bandabichi kuwa utaleta mapinduzi ya kiuchumi kwa jamii
Alisema TARURA Wilayani Iringa wamefanikiwa kutekeleza kwa vitendo azma ya serikali ya awamu ya sita katika kuchochea maendeleo ya haraka kwa wananchi huku akiwahimiza wananchi kuitunza miundombinu hiyo
Lakini pia Dr. Nyamahanga aliipongeza serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi mkoa wa Iringa kwa ajiri ya maendeleo ya ujenzi wa barabara na madaraja mkoni humo
Kiongozi huyo wa CCM mkoa wa Iringa wakati wa ziara hiyo amepokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa barabara Na daraja la Ifunda Bandabichi, huku akisema kuwa daraja hilo ni mkombozi wa Kiuchumi kwa wananchi wa maeneo hayo
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Iringa Barnaba Selemani Jabir aliyebainisha gharama za mradi wa ujenzi wa barabara ya Ifunda Itengulinyi pamoja na madaraja mawili moja likiwa ni watembea kwa miguu umegharimu kiasi milioni 984
Kukamilika kwa mradi huo kunatajwa kuwanufaisha wakazi wa takribani kata tano ikiwemo Kata ya Ifunda, Lumuli, Maboga, wasa na Tungamalenga za wilayani huo.
Meneja wa TARURA Barnaba Selemani Jabir ameipongeza na kuishukuru Serikali kwa kuboresha bajeti ya TARURA na kuitaja kuwa na tija kwa wilaya
Vumilia mwenda diwani wa viti maalum Tarafa ya Kiponzero ameeleza maswahibu yaliyokuwa yakiwakabili waananchi waliokuwa wakilazimika kuvuka mto uliopo eneo hilo kabla ya ujenzi wa daraja.
Alisema kabla ya ujenzi wa barabara hiyo wananchi wengi walikuwa wanalazimika kuvua nguo kwanza ili waweze kuvunga mto huo hivyo ujenzi wa daraja hilo umekuwa mkombozi kwa wananchi wa zaidi ya kata tano ambao wanatumia kupita katika barabara hiyo.