Home Mchanganyiko SHILINGI BILIONI MBILI KUKARABATI MITAMBO YA UJENZI WA SKIMU ZA KILIMO CHA...

SHILINGI BILIONI MBILI KUKARABATI MITAMBO YA UJENZI WA SKIMU ZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

0

 

Na Mwandishi Wetu –
Dodoma

Kiasi cha fedha shilingi Bilioni Mbili za kiTanzania,
zitatumika katika ukarabati na matengenezo ya mitambo inayotumika katika ujenzi
wa miundombinu katika skimu  za kilimo
cha Umwagiliaji nchini.

Hayo yamesemwa jana jioni jijini Dodoma, na kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali alipokuwa akizungumza
waandishi wa habari katika viunga vya ofisi za Tume hiyo wakati zoezi la
ukabati wa mitambo hiyo ukiendelea.

Bw. Kaali alisema nchi nzima ina mitambo zaidi ya 53 na
inayoweza kutengenezwa ni mitambo 44 na malengo yaliyowekwa na Tume hiyo ni
kutengeneza mitambo 43 hadi kufikia mwakani 2023. “Tutaokoa fedha nyingi kwani kukodi mtambo mmoja siyo chini ya Sh. Milioni moja kwa siku moja na unaweka kukuta, skimu moja inaweza ikahitaji siku hata ishirini au theathini kwa ajili ya
matengenezo , hivyo kwa mahesabu ya haraka utaona ni fedha nyingi sana zinahitaji
kukodisha mtambo mmoja kwa siku”. Alisisitiza Kaali.

Aidha aliendelea kufafanua kuwa, Tume hiyo imetenga wastani
wa hekta laki mbili na hamsini kwa mwaka zinazoweza kuendelezwa, hivyo
matengenezo ya mitambo hiyo yataweza kuongeza kasi ya kuweza kuendeleza eneo
hilo. “Tukienda hivi baada ya miaka mitano tunaweza kuwa tumeongeza eneo la
kilimo cha umwagiliaji kufikia hekta milioni moja na laki mbili. Alisema.

Mhandisi Hassan Ndyali, ni Msimamizi wa kitengo cha mitambo
hiyo anafafanua kuwa, pamoja na kuwa kazi ya kukarabati mitambo hiyo ni sehemu
ya majukumu ya ofisi, alisema kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri
wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe “Ambaye alitamani sana kuona tunafanya kazi hiyo
kwa ufanisi mkubwa na kukamilisha kwa wakati ili mitambo hiyo iweze kuleta tija
kwa Taifa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.” Alisisitiza Mhandisi Ndyali.

Mmoja wa fundi wa mitambo hiyo Bw. Raphael Kanuha,
amewahakikishia wakulima kuwa mashine hizo
zitakamilika ndani ya muda mfupi na zitaingia kazini na kufanya kazi kwa
ufanisi.

Picha Ikimuonesha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji, Bw. Daudi Kaali alipokuwa akizungumza na waandishi wa
Habari hawapo katika picha, kuhusu matengenezo ya Mitambo, katika Ofisi
za Tume ya Taifa ya Umwagilijai Jijini Dodoma jana.
Picha ikionesha moja ya mtambo uliokarabatiwa unaotumika katika ujenzi wa skimu za kilimo cha umwagiliaji.
Mhandisi Hassan Dyali akizungumza na waandishi wa habari kuhuasiana
na sehemu ya  majukumu ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ya Ukarabati wa
Mitambo inayotumika katika Ujenzi wa Skimu za Kilimo cha Umwagiliaji
nchini.

 

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0cm 5.4pt 0cm 5.4pt;
mso-para-margin:0cm;
mso-para-margin-bottom:.0001pt;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:10.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;}