Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawe Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya kitengo hicho katika kutoa huduma bora za visima na mabwawa ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa Mhandisi Simon Ngonyani akiwasikiliza wafanyakazi wa kitengo hicho katika hafla ya kujitambulisha katika kuanza kazi ofisii hiyo,jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Kitengo cha Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo hicho Mhandisi Simon Ngonyani hayupo pichani ,jijini Dar es Salaam.
***************************
*Ngonyani atoa mikakati ya utoaji huduma bora za uchimbaji visima na ujenzi wa Mabwawa
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI inatarajia kuagiza mitambo mikubwa ya kisasa 25 ya uchimbaji visima na seti tatu ya mitambo ya kujenga mabwawa lengo likiwa ni kutoa huduma kwa wananchi mjini na vijijini na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es salaam Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa Mhandisi Simon Ngonyani amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi wengi mjini na vijijini kwa kuwa na visima bora pamoja na mabwawa
Ngonyani amesema kuwa kitengo hicho kilijulikana zamani Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA)hivyo sasa ni kitengo kilicho chini ya Mamlaka ya Vijijini na Mijijini (RUWASA)
Amesema kumekuwa na vishoka wa uchimbaji visima na mabwawa hali ambayo imefanya wananchi kuwa na visima na mabwawa yasiyo na viwango wakati mwingine maji hayo yanakuwa hayana ubora kwa matumizi ya binadamu.
” Hivi sasa uchimbaji visima umeingiliwa na watu ambao ni vishoka, lazima tuwaambie wananchi pamoja na taasisi ambazo zinahitaji huduma ya kuchimbiwa visima,hawana sababu ya kutangatanga mitaani waje DDCA ya zamani ambayo sasa imebadilishwa jina kwa na kuitwa Kitengo cha Uchimbaji Visima na Mabwawa tuwapatie huduma kwani kitengo chetu kina wataalam wa kutosha wenye uwezo wa kazi hiyo,” amesema Ngonyani
Ameema mwaka jana walipewa kazi na Wizara ya Maji ya kuchimba visima 500, lakini walishindwa kukamilisha kazi hiyo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mitambo ila kwa mwaka huu wanaimani watafanikiwa kuchimba visima zaidi baada ya serikali kuagiza mitambo hiyo katika kutoa huduma bora
Ngonyani amesena kuwa sasa wakala uchimbaji visima na mabwawa watanfanya kazi ya kutoa huduma bora kutokana na kuwa na wataalam.
Ngonyani, alitahadhrisha wananchi,taasisi za umma na serikali kuacha kutumia vishoka kwani hawana utaalam. “Kwa mfano ukiangalia kwa hapa Dar es salaam, utakuta visima vingi vimechimbwa karibu na miundombinu ya majitaka na kusababisha magonjwa ya milipuko. Kumbe watu wanatumia maji yanayoingiliana na mfumo wa maji machafu,” alisema na kuongeza kuwa;