Ofisa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Mary Mwasikili, akizungumza na mmoja wa wateja walioshinda katika droo ya pili ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa na kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Mfuru. (Na Mpiga Picha Wetu).
Meneja Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa, akibonyeza kitufe cha kompyuta kutafuta washindi wa droo ya NMB MastaBata Kivyako Vyako iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Mary Mwasikili na kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Mfuru. (Na Mpiga Picha Wetu)
…………………………..
KAMPENI ya ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako’, inayoendeshwa na Benki ya NMB imeezidi kushika kasi ambako wateja 100 wa Benki hiyo wametangazwa washindi wa Sh. Milioni 10 za droo ya wiki ya pili.NMB MastaBata ni kampeni inayolenga Kuhamasisha Matumizi na Malipo kwa njia ya MasterCard, Masterpass QR na PoS, ambako NMB imetenga zaidi ya Sh Mil. 200 zinazoshindaniwa katika kipindi cha wiki 10, huku washindi wakipewa pesa taslimu ili kuwapa uhuru wa kujipangia matumizi.Akizungumza kabla ya droo ya Wiki ya Pili iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kitengo cha Kadi wa NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema kampeni hiyo inapewa msukumo wa mahitaji ya ulimwengu wa kisasa unaoamini katika matumizi yasiyohusisha pesa taslimu, ambayo yanakabiliwa na changamoto kadhaa, zikiwamo za upotevu na wizi.Aliongeza kuwa, kutokana na uhitaji huo, NMB wakabuni kampeni hiyo ambayo imefanyika kwa misimu mitatu sasa na kuchagiza ukuzaji wa matumizi ya kadi, kiasi cha benki yake kutunukiwa Tuzo ya Benki Kinara wa Uhamasishaji Matumizi ya Kadi mwaka 2021, ambako walikuza matumizi hayo kwa asilimia 104.“Kampeni hii ilianzishwa mwishoni mwa Desemba mwaka jana na itaendelea kwa wiki 10, ambako zaidi ya washindi 1,000 watazawadiwa pesa taslimu. Tutakuwa na washindi 100 wa kila wiki, washindi 25 wa kila mwezi ambao watajishindia Sh. 100,000 kila mmoja, na katika ‘Grande Finale’ tutatoa washindi 30 wa Sh. Mil. 3 kila mmoja.“Wito kwa wateja wetu ni kuendelea kutumia kadi zao kufanya malipo na matumizi kwa MasterCard, Masterpass QR na Vituo vya Malipo vya NMB (PoS), ili kujiongezea nafasi za kushinda. Wasio na kadi waziombe matawini na wasiokuwa wateja wetu, watembelee matawi yetu kote nchini wafungue akaunti, ili sio tu kushinda zawadi hizi, bali pia kufurahia huduma zetu,” alisema Mwamwitwa.NMB MastaBata – Kivyako Vyako inafanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ambapo droo ya pili ilikuwa ikisimamiwa na Pendo Mfuru, aliyewahakikishia wateja wa NMB kuwa vigezo na masharti vinazingatiwa katika kupata washindi wa kampeni hizo.“Jukumu letu kubwa ni kusimamia michezo hii na niko hapa kwa jukumu hilo na niwahakikishie wateja wote kuwa kila kitu kinaenda chini ya utaratibu, sheria na kanuni za GBT,” alisema Pendo Mfuru kabla ya kuanza uchezeshwaji wa droo hiyo ya pili.