MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,amsikiliza Mkuu wa shule ya Sekondari ya Msanga Hatibu Luwumba wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 katika shule hiyo iliyopo wialayani Chamwino mkoani Dodoma wakati wa zaira ya kukabidhi madarasa pamoja kuzindua vyumba vya madarasa.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na wananchi wa Msanga (hawapo pichani) wakati wa kukabidhi pamoja na kuzindua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 katika shule ya Msanga wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Fatuma Mganga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
WANANCHI wa Msanga wakifatilia uzinduzi wa vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 katika shule ya Msanga wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizundua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 katika shule ya Msanga wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa amekaa ndani ya darasa mara baada ya kuzindua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 katika shule ya Msanga wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya,akimpongeza Mkuu wa wa Dodoma Anthony Mtaka,mara baada ya kuzindua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC),Mkoa wa Dodoma,Ismail Jama,wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ya kuzindua vyumba vya madarasa katika wilaya ya Chamwino.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizundua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Chamwino yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akimsikiliza Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa amekaa ndani ya darasa mara baada ya kuzindua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akimsikiliza Mkuu wa Shule ya Msingi Shikizi ya Mizengo Pinda Mwalimu Mary Linje akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa ujenzi wa madarasa wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule hiyo yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akitoa maagizo mara baada ya kuzindua vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Shikizi ya Mizengo Pinda yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akisalimiana na wanakikundi wa ngoma mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari MAnchali kwa ajili ya kuzindua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akipiga ngoma mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Manchali kwa ajili ya kuzindua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akisikiliza taarifa fupi ya ujenzi wa madarasa iliyosomwa na Mkuu wa Sekondari Manchali Mwalimu Gwaje Peter wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa pamoja na wananchi wakizindua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Manchali yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Muonekano wa Madarasa yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari Manchali yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Chamwino
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka wazazi wilayani Chamwino kuwakupeleka watoto shule na kuacha kisingizio cha kutokuwa na vifaa vya shule badala yake waende hivyohivyo wakati wao wakiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya vifaa hivyo.
Mtaka ameyasema hayi wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati wa zaira ya kukabidhi madarasa pamoja kuzindua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na Uviko 19.
Shule hizo za Sekondari ya Manchali, Msanga, Buigiri na Chamwino, zilikabidhiwa Sh 60 milioni kila moja mwaka 2020 ikiwemo na shule shikizi ya Mizengo Pinda iliyokabidhiwa Sh milioni 40 zimenufaika na ujenzi wa madarasa, madawati na Ofisi za walimu.
“Hatuwezi kujenga madarasa haya yote alafu utuletee habari ya kukosa sjui nini,,, hana uniforom (sare) peleka hivyohivyo, hana kiatu aende darasani, vitakuja akiwa hukohuko kwahiyo hakuna kisingizio, atakaposoma atajifunza kununua kiatu chake”amesema Mtaka
Hata hivyo ,Mataka ameipongeza serikali kwa mradi huo na kwamba wananchi wahakikishe hakuna mtoto anaebaki nyumbani bila kusoma.
Hata hivyo Mkoa wa Dodoma ulikabidhiwa Sh bilioni 15.5 kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa, ofisi na madawati kupitia Fedha za kyupambana na Uviko 19 ambapo kwenye wilaya ya Chamwino walikabidhiwa Sh 2 bilioni kujenga madarasa 146.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya amesema kuwa Serikali ilitoa shilingi bilioni 2.92 za mradi wa UVIKO-19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 146 katika Halamashauri ya wilaya hiyo.
Pia wananchi wa Halamashauri ya hiyo wametakiwa kuwahamashisha watoto wao kusoma katika madarasa hayo yaliyojengwa kwa mradi wa UVIKO-19 ili yalete tija.
Msuya amesema moja ya Halmashauri iliyopata fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ni Wilaya ya Chamwino.
Msuya amesema kuwa Wilaya hiyo imewekewa bajeti kubwa katika mradi wa ujuenzi wa madarasa ambayo inatokana na fedha za UVIKO-19.
“Nampongeza serikali kwa ujenzi huu wa madarasa pia naishukuru kwa kutupatia Halmashauri yetu shilingi bilioni 2.92 hili ni jambo la kujivunia,” amesema Msuya
Aidha amewapongeza wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuwa walinzi wa vifaa vya ujenzi pamoja na miundombinu.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari ya Msanga Hatibu Luwumba amesema shule hiyo imepewa kiasi cha shilingi milioni 60 na kwamba wananchi walichangia milioni 1.6.
Pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma (CCM),Godwin Mkanwa amesema mafundi wanaojenga madarasa kupitia mradi wa UVIKO-19 wamejengewa uwezo.
Amesema katika ujenzi wa madarasa katika kata ya Msanga nidhamu ya matumizi ya fedha hizo yamekuwa ni ya nidhamu kubwa.
“Nawapongeza wananchi na viongozi wa Wilaya hii katika kujitolea kuchangia ujenzi wa madarasa,” amesema.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa Shule ya Manchali mkuu wa Shule hiyo Gwaje Peter amesema kuwa wananchi walijitolea kuchimba msingi, kuleta kokoto, mawe na vifusi ambapo shughuli hizo ziligharimu Sh 2860,000.
Aidha shughuli hizo pia zilifanywa na wananchi katika shule ya Sekondari Msanga ambapo walichangia jumla ya Sh 1600,000, shule ya Buigiri Sh 3080,000, na shule shikizi ya msingi Mizengo Pinda Sh 3134500.