Meneja wa RUWASA  Mkoa wa Dodoma  Dk. Godfrey Mbabaye,akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa miradi ya maji  wakati  wa hafla fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA)Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati  wa hafla fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA)Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Fatuma  Mganga,akizungumza wakati  wa hafla fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA)Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,,akizungumza wakati  wa hafla fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA)Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati  wa hafla fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA)Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akishuhudia utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA)Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Meneja wa RUWASA  Mkoa wa Dodoma  Dk. Godfrey Mbabaye,(kulia) akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kharton Traders Limited Karim Jiwa mara baada ya kusaini  mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA)Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Meneja wa RUWASA  Mkoa wa Dodoma  Dk. Godfrey Mbabaye,akibadilishana mkataba na Mkurugenzi wa Hamwa Construction Mhandisi Zinga Mohamedi mara baada ya kusaini  mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA)Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAKANDARASI wanaotekeleza miradi ya maji kwa kutumia fedha za UVIKO-19,wametakiwa kukamilisha kwa wakati na kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati  wa hafla fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kati ya makandarasi na  mamlaka ya maji  vijijini (RUWASA) Mkoa wa Dodoma.

Amesema kwa mkandarasi atakaye tekeleza miradi hiyo chini ya kiwango na nje ya mkataba Mkoa hautampatia kazi nyingine tena.

“Niseme tu kwamba kwa mkandarasi  atakayeshindwa kutekeleza miradi yake kwa muda na kwa ufanisi hatutampatia kazi tena (tutamblacklist)  kwani lengo ni kwamba kwenda na kasi ili kazi zikamilike mapema”amesema Mtaka

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Fatuma  Mganga amesisitiza miradi hiyo ifanyike kwa ufanisi na kwa kiwango cha thamani ya fedha iliyotolewa ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Awali akisoma taarifa fupi ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa Meneja wa Ruwasa Mkoa  Dr Godfrey Mbabaye amesema mikataba inayosainiwa imegawanyika katika makundi mawili.

Amesema mkoa wa Dodoma ulitengewa kiasi cha shilingi billion 3.9 kutekeleza miradi 8 katika Wilaya za Kongwa,Chamwino,Kondoa Chemba na Mpwapwa.

“Mikataba inayotarajiwa kusainiwa leo ni mikataba miwili ya Wilaya za Chamwino,Chemba  na Kondoa yenye jumla ya miradi mitano ambapo thamani ya mikataba hiyo ni shilingi bilioni 1.9”amesema Mbabaye.

Amesema mkataba mmoja wenye miradi mitatu ya Wilaya ya Kongwa,na Mpwapwa wenye thamani ya shilingi billion 1.6 umepelekwa kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali kwaajili ya kufanyia upembuzi na unategemewa kusainiwa kabla ya January 16 2022.

“Miradi inayotumia fedha za ndani inayotegemewa kusainiwa leo ni miwili ambayo itatekelezwa katika wilaya za Chamwino na Kondoa na miradi hiyo inajumla  ya shilingi bilioni 1.7” amesema Mbabaye