NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.
Baraza la Taifa la simamizi wa mazingira (NEMC) limetoa siku tatu kwa dereva wa roli aliye mwaga kemikali ya Salfa katika eneo la Msimba Tarafa ya Mikumi Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro kujisalimisha baada ya kemikali hiyo kuanza kuleta madhara kwa wananchi waliokaribu na eneo hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC) Jamali Baruti ametoa siku hizo baada ya kufika na kujionea namna wananchi wa eneo hilo walivyo athiriwa na Kadhia hiyo.
NEMC imefikia hatua hiyo baada ya kupata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo, huku wananchi wakianza kupata madhara ikiwemo kumwa macho ,vichwa pamoja na kuashwa kwa ngozi.
Amesema NEMC imesikitishwa na kitendo cha dereva wa roli hilo aliyekuwa akitokea Dar es salaam kuelekea nchi ya jirani ya Kongo kumwaga kemikali na kutokomea kusikojulikana.huku ikiwa bado aijafahamika chanzo cha kuwepo kwa salfa hiyo iwapo ni ajali ama laa
Katika hatua nyingine NEMC itamfuatilia na kumchukulia hatua dereva kwa kufuata sheria za mazingira,kwani kitendo alichokifanya ni uharibufu wa mazingira huku wahanga wakubwa wakiwa ni wananchi waishio jirani na eneo hilo kwani kemikali hiyo inamadhara makubwa kwa binaadamu na mazingira kwa ujumla.
Sambamba na hayo NEMC inatoa rai kwa madereva wanaoendesha magari ya mizigo hususani wanaobeba kemikali kufuata kanuni na miongozo ya ufungaji wa mizigo pamoja na kutumia vifungashio vinavyokizi vigezi.
Kwa upande wao wananchi ambao ni mashuhuda wa tukio wamesema roli hilo lilidondosha kemikali hizo usiku wa januari mosi 2022 na kusababisha madhara kwa wananchi ikiwemo kuumwa na kichwa,macho na kifua hali ambayo imeleta sintofahamu kwa wakazi hao kwa kuhofia afya zao na kutokujua nini cha kufanya.
Aidha walisema ukosefu wa elimu ndio chanzo cha kuathiriwa na kemikali hizo huku wakiiomba serikali kuwasaidia kupata matibabu ya haraka kunusuru afya zao.