Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini akizungumza na mamia ya Wakazi wa Songea Mjini waliojumuika kwa pamoja katika Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila ili kusherekea sikukuu ya Mwaka Mpya ikiwa ni jitihada za kuhamasisha utalii wa ndani
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini akiwa na Meya wa Manispaa ta Songea Mjini, Mhe.Michael Mbano wakiwa wameongozana na Wakazi wa Songea Mjini mara baada ya kuwasili katika Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila iliyopo katikati ta Manispaa ya Songea ikiwa ni muendelezo wa kuukaribisha mwaka mpya kwa kuhamasisha wakazi wa Songea kujenga utamaduni wa kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Muendesha baiskeli wakijiandaa kuanza mashindano ya baiskeli yaliyofanyika ndani ya Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini, Dkt.Damas Ndumbaro akiendesha baiskeli ndani ya Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila katika mashindano yaliyofanyika katika Bustani hiyo ikiwa ni jitihada za Dkt.Ndumbaro za kuhamasisha utalii wa ndani kwa Wakazi wa Songea Mjini
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhiwa zawadi ya saa ikiwa ni kutambua na kuthamini jinsi anavyojali na kuzingatia muda licha ya kuwa na majukumu mengi yanayomkabili katika hafla ya kuhamasisha utalii iliyofanyika ndani ya Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila ikiwa ni jitihada za kuhamasisha utalii wa ndani kwa Wakazi wa Songea Mjini
Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi wa Kanda ya Kusini ya TAWA, Abraham Juru akimkabidhi zawadi maalumu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma, Mhe.Odo Mwisho aliyeibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika ndani ya Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila ikiwa ni jitihada za kuhamasisha utalii wa ndani kwa Wakazi wa Songea Mjini
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini, Dkt.Damas Ndumbaro ( kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma, Mhe.Odo Mwisho wakati wa siku ya pili ya Sikukuu ya mwaka mpya zilizofanyika ndani ya Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila ikiwa ni jitihada za kuhamasisha utalii wa ndani kwa Wakazi wa Songea Mjini
Moja ya jiko la nyamapori iliyoandaliwa kwa ajili ya Wakazi wa Mji wa Songea katika sherehe za kuukaribish mwaka mpya ikiwa ni jitihada za Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro za kuhamasiaha na kujenga utamaduni kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kutembelea vivutio vya utalii
…………………………………………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wana kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo kutoa fedha kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii za kukarabati miundombinu ya maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo katika Mkoa huo.
Wito huo ameutoa wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jimbo la Songea mjini kwenda kusheherekea mwaka mpya wa 2022 kwa kufanya utalii wa ndani kwa nyakati tofauti katika Msitu wa Hifadhi ya Mlima Matogoro pamoja na Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila iliyopo katikati ya Manispaa ya Songea Mjini
Akitaja fedha manufaa ya fedha hizo, Dkt.Ndumbaro amesema Songea ni mji uliobarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii hivyo fedha hizo za mkopo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya maeneo ya vivutio ili kuimarisha utalii
Amesisitiza kuwa Hifadhi ya Msitu wa Mlima Matogoro ni kivutio kikubwa cha utalii katika mkoa huo isipokuwa changamoto ya barabara ndiyo imekuwa kikwazo cha watalii walio wengi kushindwa kufika
Dkt.Ndumbaro amesema kupitia fedha hizo za mkopo itajengwaa barabara ya uhakika itakayofika hadi juu ya misitu ya milima Matogoro ili kuwarahisishia wanaoenda kufanya utalii huku akisisitiza kuwa tayari Mkandarasi amepatikana na anatajiwa kukabidhiwa eneo la ujenzi tarehe 15 Januari mwaka huu
” Mhe.Rais ametuona na kutuamini wana Songea kwa kutupatia fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara ili kuhakikisha watalii watakaoamua kutumia magari yao kufika katika kilele cha Mlima huo wanaweza kufika tofauti na ilivyosasa magari madogo huku hayawezi kufika kutokana na ubovu wa barabara” alisema Dkt.Ndumbaro
Pia, Dkt.Ndumbaro amesema Mhe.Rais Samia Samia aliridhia kutengwa kwa bajeti ya mwaka huu ya jumla ya kiasi cha shilingo milioni 50 kwa ajili ya kukarabati uzio wa Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila.ambayo imezidi kupata umaarufu siku za hivi karibuni baada ya kufanyika kwa maboresho makubwa
Dkt Ndumbaro amesema kuboreka kwa miundombinu katika maeneo ya vivutio vya utalii kutachochea Manispaa ya Songea mjini kimapato.kwa vile Utalii ni sekta mtambuka
Hata hivyo, Dkt.Ndumbaro amewataka Wakazi wa Songea kuchangamkia fursa za utalii zilizopo katika mkoa huo huku akiwasisitiza kujenga tabia ya kutembelea maeneo ya vivutio hivyo ili kutambua fursa zilizopo kwenye maeneo yao.
Katika hatua nyingine Waziri Ndumbaro amewataka Wananchi hao kuwa mstari wa mbele kulinda na kuhifadhi maeneo ya vivutio vya utalii badala ya kuiachia Wizara pekee ili maeneo hayo yaweze kuchochea kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia sekta ya utalii.
Katika kusherehekea sikukuu ya Mwaka mpya katika Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila, Waziri Ndumbaro aliweza kuwalipia wakazi wote wa Songea Mjin i tozo zote za vingilio katika Bustani hiyo pamoja na kuhakikisha wanakula nyama pori iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya wakazi hao