Na.Alex Sonna,Bahi
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ally amewataka wazazi na walezi kutoa fursa kwa watoto wa kike ya kupata elimu na kuacha kuwaonzesha mapema ili kujenga Taifa lenye Kizazi bora.
Akizungumza wakati wa mbio za mwenge katika Halmashauri ya wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipokuwa akizindua mradi wa umaliziaji wa maboma ya madarasa manne katika shule ya sekondari Mndemu Mkongea amesema watoto hao wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.
Mbali na hayo amewataka wananchi kushirikiana na Serikali katika kutunza mazingira na kuacha kukata miti ovyo, ameyasema hayo alipotembelea mradi wautunzaji maji na uhifadhi wa msitu wa Chenene.
Mara baada ya kukangua na kupokea miradi hiyo amewataka wananchi kuendelea kuboresha miundombinu hiyo ili kuweza kujipatia maendeleo na kwenda sambamba na kasi ya Rais John pombe magufuli.
Mbali na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo, Mwenge wa Uhuru 2019 uliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya km 2.3 katika mji wa Bahi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyowahi kuitoa Rais dkt John Magufuli wakati wa kampeni 2015, uliweka jiwe la msingi mradi wa usambazaji maji kijiji cha Mkakatika na kutembelea ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Bahi.
Aidha mwenge huo ulitembelea mradi wa utunzaji wa chanzo cha maji na uhifadhi wa msitu wa Chenene uliopo kijiji cha Mayamaya, uliweka jiwe la msingi mradi wa kuzalisha kokoto katika kiwanda cha kokoto cha kampuni ya KASCCO miradi yote 6 imeghalimu Tsh bil 8.7.