Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Yasinta Mwandelele wa Mtandao wa mazao yanayotokana na samaki wakati aliipotembelea banda la mtandao huo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salam, Desemba 11, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salam, Desemba 11, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua mpango wa ‘Women Mean Business Program’ Kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Desemba 11, 2021. Kushoto ni Waziri wa chi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Geofrey Mwambe, Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Angelina Mgalula na wa pili kulia ni Hellen Fytche, Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano,Ubalozi wa Canada nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salam, Desemba 11, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF Bw. Francis Nanai akizungumza katika mkutano Mkuu wa 21 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) uliofanyika Chuo Kikuu cha (UDSM) Jijini Dar es Salaam.
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Ummy Mwalimu akitoa salamu zake katika mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha UDSM jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Angelina Ngalula akitoa hotuba yake katika mkutano mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) uliofanyika Chuo Kikuu cha (UDSM) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Angelina Ngalula kulia na Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Ummy Mwalimu wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wafanyabiashara washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
Serikali imesema kuwa itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ikiwemo kushiriki miradi ya kimkakati ili iweze kuinua wafanyabiashara nchini.
Hayo ameyasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akifungua mkutano Mkuu wa 21 wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) uliofanyika Jijini Dar es Salaam ,amesema kuwa sekta binafsi inatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ikiwa ni pamoja na kuweka fedha katika benki na sio kuzifungia ndani.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa kwa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Benki Kuu kuangalia namna ya kupunguza riba ili kufanya biashara ziweze kukua pamoja na kubaki na fedha za kuendesha biashara hiyo.
Amesema kuwa vitu vilivyokuwa vikwanzo wameweza kuondoa tozo ikiwa ni nia ya serikali kuhakikisha sekta binafsi inakua kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Aidha amesema kuwa katika kufanya biashara kwa sekta binafsi waende kuwekeza hadi maeneo ya vijijini kutokana na serikali kuweka huduma ambazo ni wezeshi kwa kufanya biashara.
Hata hivyo Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Nishati na Wizara ya Maji kuhakikisha wanapeleka huduma za maji na nishati kwa maeneo yanayowekeza ili isiwe kikwazo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Taasisi za Udhibiti TBS,TMDA ,Ardhi kuwa na dirisha la pamoja katika ofisi za mikoa katika kurahisisha kuondoa usumbufu kwa wawekezaji pindi wanapotaka kuwekeza.
Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Angelina Ngalula amesema kuwa serikali isaidie kuwashika mkono wafanyabiashara kuweza kufanya biashara ndani na nje ya nchi kama ambavyo nchi zingine zinavyofanya.
Mwenyekiti Ngalula amesema kuwa katika miaka 21 ya TPSF serikali imeweza kuondoa vikwazo zaidi ya 40 hali ambayo imefanya sekta binafsi kuendelea na kutoa mchango kwa nchi pamoja wananchi.
Ngalula amesema sekta binafsi inaendelea katika kujiimarisha na kuongeza wanachama ambapo ni kutaka kuendelea kukua zaidi kwa kutanua uwigo wa biashara.
Amesema wanamshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kufungua milango na mataifa mbalimbali.