*************
Na Stahmil Mohamed
Wito umetolewa kwa wananchi, taasisi binafsi na kampuni mbalimbali nchini kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu.
Wito huo umetolewa leo na Mmoja wa waasisi wa harakati za uchangiaji damu Bw Semeni Kingaru katika kituo cha uchangiaji damu cha Msimbazi center jijini Dar es salaam ambapo taasisi ya Family Federation for world peace inayoshughulika na kupambana na mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii ili kujenga taifa la wazalendo wameshiriki kuchangia damu lengo hasa kuwasaidia majeruhi mbalimbali walionusurika katika ajari ya moto baada ya gari lilokuwa likisafirisha mafuta kupinduka na kusababisha mlipuko wa moto Nakuweza kusababisha takribani vifo vya watu 80 na majeruhi zaidi ya 70 nanenane mjini Morogoro .
Kingaru ameendelea kwa kusema kuwa takribani watu 70kutoka taasisi ya Family Federation wamejitokeza Leo kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu pia ameongeza kuwa Maadhimisho ya utoaji Damu kwa Dar es salaam itakuwa tarehe 31 mwezi wa nane 2019 ambapo watakusanyika wanandoa 80,000 pale uwanja wa Taifa Dar es salaam kwa ajili ya Tamasha ambapo wanatarajia mgeni rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt john pombe Magufuli.
Hata hivyo Kingaru ameongeza kuwa taasisi ya Family Federation itaendesha zoezi endelevu la uchangiaji damu Kwani Dar es salaam peke yake wana Familia 100,000 hivyo wanampango kuzunguuka Nchi Mzima kwa ajili ya kutoa elimu ya upendo na amani na kujitoa kwa ajili ya wengine
Dismas Chikawe na Joseph Michael ni baadhi ya wanachama kutoka Family Federation ambao wamejitokeza kuchangia damu wanaeleza umuhimu wa uchangiaji Damu kwani inasaidia kuokoa maisha ya watu mbalimbali wenye uhitaji wakiwemo majeruhi wa ajali mbalimbali,wanawake wanaoenda kujifungua n.k.
Kwa upande wake Secilia Afred Meela ambaye ni muhudumu wa utoaji damu katika kituo cha Msimbazi Centre ameishukuru taasisi ya family Federation kwa kushiriki katika utoaji damu na kutoa rai kwa wananchi, taasisi mbalimbali kujitokeza kuchangia damu kwani kuna upungufu mkubwa wa damu nchini.
Zoezi hili la utoaji damu ni endelevu nchini lengo ni kusaidia watu mbalimbali wenye uhitaji wa damu hasa majeruhi wa ajali ya Moto kutoka mkoani Morogoro