Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa ziara ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan
………………………………………………..
Na Victor Masangu,Pwani
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kuzindua kiwanda kipya Cha kisasa Cha Raddy Fibre Manufacturing kilichopo Wilayani Mkuranga kinachotengeneza nyaya za mawasiliano kwa ajili ya mkongo wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema kuwa kiwanda hicho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa mkuranga pamoja na Taifa zima kwa ujumla.
Kunenge alisema kuwa kiwanda hicho ambacho ni Cha nne kwa ukumbwa barani afrika kitakuwa ni chachu ya kukuza uchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo sambamba na kukuza teknolojia ya mawasiliano.
Aidha Kunenge alimpongeza Rais Samia kwa kuamua kufanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Mkuranga na kuamua kwenda kufanya uzinduzi wa kiwanda hicho ambacho kitaweza kuliletea heshima taifa la Tanzania.
Alifafanua kuwa kukamilika kwa kiwanda hicho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga kuweza kupata fursa mbali mbali za ajira na kuwasaidia wananchi kutoka maeneo mengine ya jirani.
Kadhalika alielezea kuwa kwa Sasa lengo la Mkoa wa Pwani nj kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya kwa lengo la kuwavutia wawekezaji mbali mbali Kuja kuwekeza katika sekta mbali mbali ili kuweza kukuza kasi ya uchumi.
Katika hatua nyingine Kunenge aliongeza kuwa katika ziara hiyo Mhe.Rais atasimama na kuzungumza na wananchi wa eneo la Vikundi na kuwataka wananchi wa mkuranga kujitokeza kwa wingi katika kwa ajili ya kumpokea.
Kunenge pia aliongeza kuwa katika uzinduzi huo utahudhuliwa na viongozi mbali mbali pamoja na baadhi ya wawekezaji mbali mbali sambamba na viongozi wa Chama na dini.