LIVERPOOL imeibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Goodison Park Jijini Liverpool usiku wa kuamkia leo.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Jordan Henderson dakika ya tisa, Mohamed Salah mawili dakika ya 19 na 64 na Diogo Jota dakika ya 79, wakati la Everton lilifungwa na Demarai Gray dakika ya 38.
Hicho kinakuwa kipigo cha kwanza kikali kwa Everton kwenye derby Merseyside nyumbani ndani ya miaka 39.
Liverpool inafikisha pointi 31, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Manchester City na mbili na Chelsea baada ya timu zote kucheza mechi 14, wakati Everton inabaki na pointi zake 15 za mechi 14 pia nafasi ya 14.