BAO pekee la mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 52 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya sita, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake mbili baada ya timu zote kucheza mechi saba na kuendelea kushika mkia.