Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivalishwa Beji kama ishara ya
kukabidhiwa Uenyekiti wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika kutoka kwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Rais wa Namibia
Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob katika mkutano uliofanyika ukumbi wa
Julius Nyerere International Convention Centre JNICC jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa
Palamagamba Kabudi pamoja na Wakuu mbalimbali wa nchi za SADIC
wakati wa wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa kabla ya kuaza kwa
mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADIC)
Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Wake wa
Marais pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania
wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya ufunguzi
wa mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) akihutubia
katika mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda wake Rais wa
Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob akifurahia jambo na Rais wa
Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa katika mkutano wa wa 39
wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika SADC mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wa 39 wa Wakuu
wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Ndani cha
Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADIC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa
Zimbabwe Mheshimiwa Emerson Mnangagwa kwa ajili ya kikao cha
Wakuu wa Nchi za SADC jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu
wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa mara baada ya kuhutubia katika
wa mkutano wa wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete na
kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi .
PICHA NA IKULU