***************
Mwili wa Marehemu baba yake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe, Sheikh Mohamed Bashe umepumzishwa usiku huu katika Makaburi ya Waislamu Kitongo Mjini Nzega Mkoani Tabora.
Akizungumza kwa niaba ya familia Mhe. Bashe amesema familia inashukuru mchango wa jamii ya wakazi wa Nzega kwa namna walivyojitokeza kushiriki na familia katika mazishi hadi maziko ya baba yake.
Kabla ya mazishi imefanyika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Sheikh Bashe iliyoswaliwa katika Msikiti wa Ijumaa mjini Nzega.
Marehemu Sheikh Mohamed Bashe alifariki Novemba 23, 2021 nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.