Jumuia ya Chuo Kikuu Mzumbe leo wamejitokeza kuungana na Wananchi wengine wa Mkoa wa Morogoro kuchangiaji damu kwa ajili kuwasaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo imefikia 89.
Idadi ya Wanajumuiya wa Chuo hicho walioshiriki kwenye zoezi la kutoa damu ni 30, ambapo wamewataka Wananchi na Taasisi nyingine kuendelea kujitokeza kwa wingi kusaidia majeruhi wa ajali hiyo, wakati jitihada za madaktari za kuokoa maisha yao zikiendelea.
Maafisa wa Chuo Kikuu Mzumbe kutoka kushoto ni Bw. Lunodzo Mwinuka na Bw. Peter Sheiza wakipata ushauri kabla ya kushiriki zoezi la uchangiaji damu Hospitali Kuu ya Mkoa wa Morogoro.
Wakiendelea na hatua za uchangiaji damu ni Bw. Wambura Magesa (kulia mwenye tisheti ya mistari) na Bw. Sasi Sasi (kushoto mwenye kofia), wote wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Bw. Ali Adrian wa kwanza kushoto akiwa na wenzake wa Chuo Kikuu Mzumbe wakichangia damu.
Bi Nuru Mbaga akiwa na tabasamu wakati akisubiri kuchangia damu majeruhi wa ajali ya lori la mafuta Msamvu Morogoro. Katika picha nyingine ni Bw. Nickson Nockodemus na Bi. Eleri Isasi nao wakiwa katika hatua za uchangiaji damu.
Akiandaliwa kwa hatua za awali za uchangiaji damu ni Bw. Hassan Lugazo wa Chuo Kikuu Mzumbe ambaye naye alishiriki kuwachangia damu majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea Jumamosi 10/08/2019 Msamvu Morogoro.
Baadhi ya Wanajumuia wa Chuo Kikuu Mzumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuchangia damu Hospitali Kuu ya Mkoa wa Morogoro.