Mratibu wa Mtandao wa wanawake watetezi wa haki za binadamu Tanzania Bi. Hilda Dadu wakati akiwasilisha ripoti ya matokeo ya uchambuzi wa mapendekezo ya miswada kuwa Sheria kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyoandaliwa na Kituo cha haki za Binadamu (LHRC) iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe.Emmanuel Mwakasaka,akizungumza wakati wa semina ya kupokea ripoti ya matokeo ya uchambuzi wa mapendekezo ya miswada kuwa Sheria kwa iliyoandaliwa na Kituo cha haki za Binadamu (LHRC) iliyofanyika jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mhe.Hawa Chakoma, akichagia mada wakati wa semina ya kupokea ripoti ya matokeo ya uchambuzi wa mapendekezo ya miswada kuwa Sheria kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyoandaliwa na Kituo cha haki za Binadamu (LHRC) iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu TAS- Chama cha watu wenye ualbino Tanzania Bw.Mussa Kabimba,akizungumza wakati wa semina ya kupokea ripoti ya matokeo ya uchambuzi wa mapendekezo ya miswada kuwa Sheria kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyoandaliwa na Kituo cha haki za Binadamu (LHRC) iliyofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kituo cha haki za Binadamu (LHRC) imetoa wito kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa kusisitiza mapendekezo ya Sheria zilizopitishwa ambazo hazijachukuliwa na kamati hiyo.
Hayo yamezungumzwa Jijini Dodoma na Mratibu wa mtandao wa wanawake watetezi wa haki za binadamu Tanzania Hilda Dadu wakati akiwasilisha ripoti ya matokeo ya uchambuzi wa mapendekezo ya miswada kuwa Sheria kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
Amesema kuwa mapendekezo yanayohusiana uzingatiaji wa usawa wa kijinsia Kama vile usawa kati ya wanawake na wanaume katika bodi au kamati zinazoanzishwa kisheria na mahitaji ya makundi Maalumu yanapaswa kuchukuliwa.
” Tunaomba na kusisitisha kamati kuangalia upya suala la adhabu za jumla pamoja na viwango vikubwa vya adhabu hizo, tunatoa wito mbele ya kamati hii kuwa utunzi wa sheria uepuke adhabu za jumla hii itawezekana endapo adhabu itokane na kifungu husika cha sheria kilichokiukwa kulingana na uzito wake” -amesema Dadu.
Hata hivyo Dadu alsema kituo hicho kinaendelea kutuma maombi kwa kamati na kuyapa uzito na msisitizo mapendekezo hayo kwa wakati ujao.
Kwa upande wa washiriki waliopata fursa ya kutoa mawazo yao baadhi yao wamesema walemavu wanapaswa washiriishwe kwenye baadhi ya nyanja muhimu ambazo zinaweza kuwaletea shida kama hawatotoa mawazo yao.
“Mfano swala la Vocha sisi walemavu wa ngozi huwa tunasumbuliwa na matatizo ya macho, unavyoona mwenyekiti sio sawa na ninavyoona Mimi, namba za vocha ni ndogo sana kam Mimi siwez kuziona lakini kama tungeshirikishwa huwenda tungetoa mawazo yetu” Alisema Mussa Kabimba katibu mkuu TAS- chama cha watu wenye ulemavu Tanzania.