Baadhi ya Wananchi wakipata maelezo ya bidhaa za TBL Katika banda la maonyesho ya Nane Nene mkoani Simiyu mapema wiki iliyopita.
Bidhaa za TDL za Konyagi na mvinyo pia zilivutia Wananchi wengi Katika maonyesho hiyo kutokana na ubora wake.
Washiriki wa Nane Nane wakifurahia bidhaa za TBL
***************
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) chini ya kampuni ya Kimataifa ya ABInBev, imeshiriki maadhimisho ya Sikukuu ya wakulima ya Nane Nane 2019, na imeeleza mkakati wake wa kuendelea kufanya kazi na wakulima kwa kuwa inaamini ili kufanikisha jitihada za serikali za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ni muhimu pia kunyanyua sekta ya kilimo kwa ajili ya kupata malighafi ya kuendesha viwanda kutoka hapa nchini.
Akiongea wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu, Meneja Mawasiliano wa TBL, Abigail Mutaboyerwa , alisema TBL Group, inaamini kuwa uwekezaji katika sekta ya kilimo ni jambo la msingi kwa kuwa utawezesha pia kunyanyua maisha ya wakulima wengi, hasa wakulima wadogowadogo ambao wanaishi maisha duni kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo matumizi ya teknolojia duni katika shughuli zao za kilimo sambamba na ukosefu wa soko la uhakika wa mazao wanayozalisha.
Mutaboyerwa, aliongeza kusema kuwa TBL kupitia mkakati wake wa kufanikisha Malengo Endelevu ya Dunia- Sustainability Goals in smart agriculture (SDGs), itaendelea kufanya kazi na wakulima kama ambavyo hatua hii imeanza kuleta mafanikio kwa kuboresha maisha ya wakulima wa Shahiri,kupanua wigo wa ajira hususani kwa vijana na Wanawake, kutokana na mpango huu na kampuni kunufaika wa kupata malighafi bora inayozalishwa hapa nchini.
“Tunao mkakati wa kubadilisha maisha ya wakulima kwa kuwawezesha kitaalamu,kiteknolojia,kuwapatia mbegu bora,mbolea,kuwawezesha kupata mikopo yenye riba nafuu na kuhakikisha mazao yao yanakuwa na soko la uhakika na bei nafuu,hii ndio njia ya kuwakomboa wakulima wadogo kutokana na uwekezaji katika sekta ya viwanda”alisema