Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mgeni Rasmi, Dkt. Buruhani Nyenzi akizungumza na wanahabari mara baada ya kutoa zawadi kwenye warsha ya TMA kwa wanahabari iliyoandaliwa maalum kujadili mwelekeo wa mvua za msimu kwa kipindi cha mwezi Novemba 2021 hadi Aprili 2022 nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi .
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (katikati) |
akizungumza na wanahabari mara baada ya zawadi kwenye warsha ya TMA kwa wanahabari iliyoandaliwa maalum kujadili mwelekeo wa mvua za msimu kwa kipindi cha mwezi Novemba 2021 hadi Aprili 2022 nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa na Meneja Rasilimali watu wa TMA, Maryam Is-haak (kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mgeni Rasmi, Dkt. Buruhani Nyenzi akikabidhi zawadi kwa mwandishi bora wa habari za TMA, Theopista Nsanzugwako kutoka Habari Leo aliyeshika nafasi ya pili leo mjini Kibaha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akishuhudia
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mgeni Rasmi, Dkt. Buruhani Nyenzi akikabidhi zawadi kwa mwandishi bora wa habari za TMA, Jerome Risasi kutoka Clouds Media aliyeshika nafasi ya kwanza leo mjini Kibaha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi
Baadhi ya maofisa wa TMA walioshiriki katika warsha hiyo
Washiriki wa warsha hiyo katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi.
……………………………….
MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), imetoa zawadi kwa wanahabari watatu wanaofanya vizuri zaidi katika uandishi wa habari zinazohusu masuala mbalimbali ya utabiri wa hali ya hewa, kwa lengo la kuielimisha jamii. Wanahabari hao wameibuka washindi baada ya kuleta kazi zao anuai walizochapisha katika vyombo vyao kuanzia mwishoni mwa mwaka jana 2020.
Wanahabari walioibuka washindi na zawadi zao kwenye mabano ni Jerome Risasi kutoka Clouds Media aliyeshika nafasi ya kwanza (Tshs 1,000,000), Theopista Nsanzugwako kutoka Habari Leo aliyeshika nafasi ya pili (Tshs 700,000) pamoja na Faustin Felician kutoka Nipashe aliyeshika nafasi ya tatu (Tshs 400,000).
Zawadi hizo pamoja na vyeti kwa washindi zimekabidhia leo mjini Kibaha na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi katika warsha ya wanahabari iliyoandaliwa maalum kuhusu mwelekeo wa mvua za msimu kwa kipindi cha mwezi Novemba 2021 hadi Aprili 2022 nchini.
Awali akizungumza wakati akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi alisema katika kuhakikisha nchi inaendelea kufikia lengo la ukuaji wa uchumi wa viwanda, TMA imeanza rasmi kutoa utabiri mdogomdogo kwa Wilaya 63 zilizopo katika ukanda unaopata mvua za msimu wa Novemba hadi Aprili kila mwaka ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda.
“Warsha hii ni muendelezo wa juhudi za TMA kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa nchini zinawafikia walengwa kwa uhakika, usahihi na kwa wakati ili ziweze kuwanufaisha,” alisema Dkt. Kijazi.
Aidha ameongeza kuwa taarifa sahihi za hali ya hewa ni muhimu kupatikana kwa wakati ili kuwezesha jamii na wadau kujipanga na kuandaa shughuli za kiuchumi na kijana katika maeneo yao.
Amesema, kupatikana kwa Utabiri kwa usahihi na kwa wakati nitachangia katika jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, nchi kwa ujumla pamoja na kuboresha miundombinu na huduma za kijamii.