Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo akieleza jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), inayoendelea Jijini Mwanza.
Baadhi ya Watoa Huduma za Afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando wakifuatilia mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), inayoendelea Jijini Mwanza.
Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana akisisitiza jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), Semina hiyo inaendelea Jijini Mwanza.
Baadhi ya Watoa Huduma za Afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Seketoure wakifuatilia mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Radenta Bahegwa akijibu hoja kutoka kwa Wataalamu wa Huduma za Afya na baadhi ya Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), mafunzo yanaendelea Jijini Mwanza.
…………………………………………………..
Na Rayson Mwaisemba WAMJW-MWANZA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yawafunda Watoa Huduma za Afya Jijini Mwanza kuwakumbusha namna ya utoaji elimu bora kwa kufuata misingi na taratibu za utoaji huduma kwa Wagonjwa ili kupunguza maambukizi mapya na vifo visivyo na ulazima.
Hayo yamejiri wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, iliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.
Katika Mafunzo hayo yaliyo andaliwa na Wizara ya Afya imedaiwa kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.
Kwa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa Wagonjwa 2577 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku Wagonjwa 1790 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.
Aidha, Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.
Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu.
Afisa Mkuu Uhakiki Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joseph Hokololo amesema kuwa zaidi ya watu milioni 1.4 Duniani wanaugua magonjwa yanayosababishwa na kupata maambukizi mapya wakati wakupata huduma ya afya, hii hutokana na Watoa huduma za Afya kutofuata taratibu za namna ya kutoa huduma.
Aliendelea kusema kuwa Asilimia 15 ya Wagonjwa hupata maambukizi ya magonjwa mapya pindi waendapo kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya, kutokana na kutofuatwa kwa taratibu, kanuni za miongozo ya kutoa huduma za Afya (IPC Guideline, SOP).
Kwa Upande wake Afisa kutoka Kitengo Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Chrisogane Justine amesema kuwa kufuata taratibu za utoaji huduma kama kanuni za uoshaji sahihi wa mikono kutamsaidia Mtoa huduma kuzuia kusambaza maambukizi ndani ya Kituo cha kutolea huduma za Afya na nje.
Licha ya changamoto za upatikanaji wa huduma za maji safi kwa baadhi ya Vituo vya Afya, Dkt. Chrisogone Justine German amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Mtoa huduma za Afya kuhakikisha ananawa mikono yake vizuri kwa sabuni na maji safi ili kuepuka kusambaza maambukizi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Akitoa Elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi mapya yanayotokea wakati wa matibabu kutokana na baadhi ya Watoa huduma kutofuata taratibu na miongozo Dkt. Radenta Bahegwa amesema kuwa asilimia 40 ya magonjwa yanayopatikana katika vituo vya kutolea huduma za Afya nayosababishwa na kutofuata kwa taratibu za miongozo ya utoaji huduma.
“Asilimia 40 ya ya magonjwa yanayopatikana katika Vituo vya kutolea huduma za Afya husababishwa na kutofuata miongozo (IPC Guidline), ndiomaana asilimia 80 ya UTI zinazoibuka katika Vituo vya Afya zinatokana na kukosea kuweka kifaa cha kupitisha haja ndogo” alisema Dkt. Radenta.
Mtaalamu kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Dkt. Alex Sanga amesema kuwa katika watu 100, watu 5 hadi 10 wanakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wa kipindu pindu, hivyo ametoa wito kwa Watoa huduma kuhakikisha wanafuata miongozo na taratibu wakati wa kutoa huduma ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi mapya katika jamii.
“Tafiti za Shirika la Afya Duniani zinonesha kuwa ndani ya miaka 3 (2015-2018) kati ya watu 33,421, watu 542 walipoteza maisha, huku katika watu 100, watu 5 hadi 10 wanakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wa kipindu pindu, hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa” alisema Dkt. Sanga.
Naye Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoa huduma za Afya jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo zingetumika katika matibabu.
Kwa upande wake Mfamasia kutoka Hospitali ya Kanda Bugando Francisco Chibunda ametoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kufuata miiko na taratibu na miongozo inavyoelekeza jambo litalosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata taratibu na miongozo wakati wakutibu ugonjwa.
“Tunapoteza nguvu kubwa, tunapoteza rasilimali nyingi kwenye dawa na matibabu, mwisho wa siku tunasababisha maambukizi mapya, nah ii hupelekea usugu wa magonjwa , kwa hiyo tubadilike” Alisema Chibunda.