WATU 10 wamenusurika kifo mmoja akiwa hajulikani alipo baada ya boti waliyopanda kuzama kwenye bahari ya Hindi Jijini Tanga wakati wakiwa wanaenda kuangalia visiwa vilivyopo majini.
Akizungumza leo na Full Shangwe Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe alithibitisha kutoka kwa tukio hilo ambapo alisema lilitokea Agosti 11 mwaka ambao walikuwa wamepanda boti waliyokodi kutoka eneo la Yanchi Club.
Alisema kwamba baada ya watu hao kupanda boti hiyo walikuwa wakienda kutembelea visiwa mbalimbali vilivyopo kwenye bahari hiyo na ndipo upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi walipotoka ndipo ilipopinduka na kuwakwaga.
“Watu hao walikuwa wametokea eneo la Yanchi Club walikuwa wanakwenda kwenye kutembelea visiwa mbalimbali vya bahari ya hindi wakati wakiwa njiani upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi wakapinduka “Alisema
Aidha kamanda Bukombe alisema kwenye boti hiyo iliyokuwa na watu 11 ambapo 10 kati yao waliweza kuokolewa kutokana na kuvaa maboya wakati wakiwa baharini na mwengine mmoja ambaye inadaiwa hakuwa nayo mpaka sasa hajulikani alipo.
“Nitoa wito kwa wananchi wanaotumia bahari kusafiria kuchukua
tahadhari wanapokuwa bahari kwa kuhakikisha wanavaa maboya ya kujiokolea ili wakati yanapotokea majanga kama hayo waweze kuona namna ya kujiokoa “Alisema Kamanda huyo.