* Watanzania
tunaamini katika kilimo na Uchumi wa Kijani
*
Kushiriki
kupanda miti ni tukio muhimu sana kwetu, ni wajibu wetu kuyalinda mazingira
PSSSF
imeungana na Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda katika
kampeni maalum ya kuhamasisha upandaji miti mkoani Dodoma inayoratibiwa na
Habari Development Association.
Akizungmza
katika hafla hiyo Waziri Mkuu mstaafu Mh. Mizengo Pinda alisema “sisi
watanzania tunaamini katika kilimo na uchumi wa kijani hivyo ni lazima tupande
miti ya kutosha ili tutunze mazingira na kupata mafanikio katika kilimo”.
Hafla
hiyo imefanyika leo Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
Mjini, Viongozi wa CCM mkoa, Mbunge wa Dodoma Mjini, Watendaji mbalimbali wa
Serikali, walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Nala na watumishi wa Mfuko
wa PSSSF.
Ujumbe
wa PSSSF uliongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSSSF, Bibi Beatrice Musa Lupi
ambaye naye alipanda miti kuashiria utayari wa Mfuko kushirikiana na Uongozi wa
Mkoa na Taasisi ya Habari Development Association katika kampeni ya kuufanya
Mji wa Dodoma kuwa wa Kijani.
Akizungumza
katika hafla hiyo Bibi Lupi alisema, PSSSF ni sehemu ya jamii ya Dodoma na
hivyo basi Mfuko una wajibu wa kuhakikisha unashiriki katika shughuli za
kijamii ikiwa ni pamoja na kupanda miti ili kuyalinda mazingira. Alibainisha
kwamba Mfuko unafahamu faida ya upandaji miti na umuhimu wa uhifadhi wa
mazingira kwa ustawi wa jamii ya wana Dodoma.
Waziri
Mkuu mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza wakati wa halfa ya upandaji miti
katika shule ya sekondari Nala, Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya
Dodoma mjini, Mhe. Jabir Shehekimweri
akizungumza wakati wa halfa ya upandaji miti katika shule ya sekondari
Nala, Dodoma
Mkurugenzi wa Fedha wa
PSSSF, Bi. Beatrice Musa Lupi
akizungumza wakati wa halfa ya upandaji miti katika shule ya sekondari
Nala, Dodoma.
mjini, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza
wakati wa halfa ya upandaji miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma
Habari Development, Bernard Mwanawile akizungumza wakati wa halfa ya upandaji
miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma
. Wanafunzi Pamoja na walimu na wageni waalikwa (picha ya chini) katika hafla
ya upandaji miti katika shule ya sekondari Nala, Dodoma, Oktoba 16, 2021.