Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kasimu Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Steven Kebwe wakati akifafanua jambao katika eneo la msavu mahali ilipotokea ajali ya moto.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kasimu Majaliwa Akimbatana Viongozi Mbalimbali Wa Kiserikali Katika wakati alipokagua eneo la ajali Msamvu Mkoani Morogoro.
Mabaki ya Lori la mafuta lililopinduka jana asubuhi mjini Morogoro na kulipuka moto.
Wananchi waliojitokeza katika uwanja wa shule ya sekondari morogoro kwa ajili ya utambuzi wa miili ya ndugu zao waliopata ajali ya lori la mafuta lililolipuka katika eneo la Msavu.
……………………………………………………..
FARIDA SAIDY MOROGORO
Waziri Mkuu wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh. Kasimu Majaliwa ameunda tume itakayochunguza chazo cha ajali ya lori lililolipuka na kuwaka moto.
Tume hiyo imeundwa leo jumapili Agosti 11,2019 ili kuchunguza kama kuna mamlaka au mtu yeyote ambaye hakuwajibika vya kutosha katika kuchukua hatua kutokana na ajali hiyo na imetakiwa kukamilisha uchunguzi huo ijumaa agosti 16 mwaka huu.
‘’Ninaunda tume ianze kuchunguza kuanzia leo hadi Ijumaa, ichambue vizuri na hata kama mimi nitakuwa sijawajibika wanitaje, baada ya hapo serikali tutajua cha kufanya.’’amesema Majaliwa.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 maeneo ya , Msamvu mkoani Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya wananchi kuanza kuchota mafuta kutoka kwenye lori hilo..
Aidha mpaka sasa Waziri mkuu amesema kuwa watu waliofariki ni 69, na majeruhi zaidi ya 66 ambapo Mh Kassim Majaliwa amewataka wanahabri kutokutoa takwimu zisizo sahihi kwani swala hilo linawatia hofu watanzania.
‘’Naogopa msije mkaingia kwenye sheria ya takwimu, kuanzia sasa chukueni takwimu sahihi kutoka vyombo vinavyohusika na za Mkuu wa Mkoa” Amesema Mh. Kassim Majaliwa.