Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma kutoka Shirika la ABT ASSOCIATES Emmanuel Malangalila akitia saini mkataba wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma awamu ya pili (PS3+), ( kulia ) ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinisia na Watoto Dk. Fatma Mrisho hafla iliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinisia na Watoto Dkt. Fatma Mrisho pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma kutoka Shirika la ABT ASSOCIATES Emmanuel Malangalila wakionesha Mikataba baada ya kutia saini mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma awamu ya pili (PS3+) hafla iliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinisia na Watoto waliohudhuria utiaji saini mkataba wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma awamu ya pili (PS3+) katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Picha na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar.
…………………………………………………………………
Na Kijakazi Abdalla ,Maelezo.
Wizara ya Afya imetiliana saini Mkataba wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma awamu ya pili (PS3+) na Shirika la ABT Associates.
Hafla hiyo ya utiaji saini ilifaywa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinisia na Watoto, Dk. Fatma Mrisho pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma kutoka Shirika la ABT Associates, Emmanuel Malangalila, katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya utiaji saini Mkurugenzi Emmanuel Malangalila alisema Mradi huo unakusudia kulenga kuboresha huduma bora kwa wananchi wanaoishi mazingira magumu.
Aidha alisema kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mradi huo pia una lengo la kuimarisha utawala bora ili kuongeza zaidi uwazi na uwajibikaji kwa wananchi katika ukusanyaji wa mapato na matumizi yake.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisema mradi huo utaimarisha mfumo wa kuandaa mipango ya bajeti na mifumo ya uhasibu ili kutoa tarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma na kupanga kukusanya matumizi bora ya rasilimali.
Sambamba na hayo, alisema mradi huo utaboresha kutumia mifumo ambayo itaweka mahusiano kwa ajili ya utawala bora ili kuhakikisha rasilimali zinakidhi mahitaji husuani kwa wanawake na vijana.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Dk. Fatma Mrisho amelishukuru shirika hilo ambalo litasaidia Serikali kuzidi kuimarisha huduma za afya Zanzibar.