Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Janet Rwegasila na Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akizindua huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa NMB, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu, Getrude Mallya.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kulia), akizindua huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Meneja Mauzo NMB, Darius Elius, Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa NMB, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu, Getrude Mallya na kulia ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Beatice Mwambije.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya WEKEZA Akaunti uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Janet Rwegasila, Mkuu wa Idara ya Bidhaa Benki ya NMB, Aloyse Maro na kulia ni Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa, Beatice Mwambije. (Na Mpiga Picha Wetu).
……………………………………………………..
MANENO MAFUPI YA MKUU WA IDARA YA BIDHAA – ALOYSE MARO KWENYE UZINDUZI WA AKAUNTI YA WEKEZA
Afisa Mkuu Wateja Wadogo na Biashara – Filbert Mponzi
Viongozi wa benki ya NMB
Wafanyakazi wenzangu wa Benki ya NMB
Waandishi wa Habari
Wageni Waalikwa
Mabibi na Mabwana
Ndugu wana habari, leo tuna jambo letu hapa, kama mnavyojua, kila siku kazi yetu ni kufikiria na kubuni mbinu tofauti yakuendelea kuwa mshirika wa wateja wetu kwenye huduma za kibenki na pia kuwaongoza namna bora ya kuhudumia akaunti zao.
Kwa maana hiyo, leo tunazindua akaunti yetu mpya, yenye lengo la kuwahamasisha watanzania kuwa na tabia ya kuweka akiba kwa muda mrefu kwa Malengo yao ya baadae.
Ikiwa na Faida zifuatazo:
- Riba kubwa ya mpaka asilimia 12 kulipwa mara mbili kwa mwaka
- Rahisi na ya haraka kuweka akiba, sehemu yoyote ulipo kupitia matawi ya NMB, mawakala wa NMB mkononi
- Bima ya Maisha Bure
Ili kuanza kujiwekea akiba hii, unatakiwa kuwa na vifuatavyo:
- Akaunti binafsi ya NMB
- Akiba kuanzia 250,000
Baada ya kusema haya machache, Naomba nimkaribishe Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara ili aseme machache na kutuzindulia akaunti yetu ya leo.
Asanteni kwa kunisikiliza