Home Mchanganyiko MATUKIO KATIKA PICHA MAKAMU WA RAIS MSIBANI KWA OLE NASHA

MATUKIO KATIKA PICHA MAKAMU WA RAIS MSIBANI KWA OLE NASHA

0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Marehemu William Ole Nasha mara alipofika nyumbani kwa marehemu Medeli – Jijini Dodoma. (Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango) Septemba 29,2021

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akimfariji Bi. Asha Mlekwa mke wa marehemu William Ole Nasha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji alipofika nyumbani kwa marehemu Medeli – Jijini Dodoma (Septemba 29,2021)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwafariji watoto wa marehemu William Ole Nasha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, alipofika nyumbani kwa marehemu Medeli – Jijini Dodoma (Septemba 29,2021)

………………………………………………………

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akiambatana na Mkewe  Mama Mbonimpaye Mpango hii leo Septemba 29, 2021 amefika nyumbani kwa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Marehemu William Ole Nasha kwaajili ya kutoa pole na kuifariji familia kufuatia kifo cha naibu waziri huyo kilichotokea Septemba 27,2021 nyumbani kwake Medeli Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais ameweka saini katika kitabu cha maombolezo na baadaye kuzungumza na Mke wa Marehemu Bi.Asha Abdallah Mlekwa   ambapo amempa pole na kumuomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

Baadaye akizungumza na waombolezaji waliojitokeza nyumbani hapo, Makamu wa Rais ametoa pole kwa wote walioguswa na msiba huo. Mamaku wa Rais amemtaja Marehemu William Ole Nasha kama kiongozi aliyekuwa hodari katika kufanya kazi zake na kuzitimiza vema. Amesema ni wazi kwamba wananchi wa Ngorongoro wamepoteza kiongozi shupavu na mwema aliyekuwa akijitoa kuwasaidia.

Aidha Makamu wa Rais amesema ni vema kujifunza juu ya Maisha alioishi Marehemu William Ole Nasha kwani yamejaa mengi yaliomema ambayo vijana wanaweza kujifunza, kuyaishi na baadae kuleta mchango chanya katika jamii