Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliyekaa kwenye Pikipiki akifurahia jambo na Mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto mara baada ya Munge huyo kukabidhi msaada wa Pikipiki mbili ili zitumike na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa. Katikati ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, ACP Juma Bwire(Picha na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi)
***************
Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Polisi, Kangi Lugola amepokea msaada wa Pikipiki amanbazo zitatumika kwa ajili ya doria ili kupunguza uhalifu Mkoa wa Iringa.
Aidha, amelitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kutotumia Pikipiki hizo kwa ajili ya kazi za kihalifu ikiwemo kusingikiza mirungi na badala yake zitumike kwa kazi iliyokusudiwa.
Lugola alitoa kauli hiyo jana, wakati akipokea msaada wa Pikipiki mbili zenye thamani ya Tsh 2.8 zilizotolewa na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto kwa ajili ya kituo cha Ikokoto Iringa.
“Tumepokea Pikipiki hizi…wazitunze ili zidumu.. zitumike kwa ajili ya kufanya doria kwenye maeneo korofi hususani maeneo ya mlima Kitonga”alisisitiza.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi na wadau werevu kuendelea kulisaidia jeshi la polisi kamwe wasichoke kutoa misaada kwa Jeshi la polisi.