Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akishiriki Jukwaa la Mawaziri wa Bara la Afrika katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani Jijini Abidjan nchini Côte d’ Ivoire leo.
**********************
Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi Jumuiya za Umoja wa Afrika ili kuendeleza utalii kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi wanachama.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani 2021 yaliyofanyika Jijini Abidjan nchini Côte d’ Ivoire leo.
“Lengo kuu la kushiriki katika Maadhimisho haya ni kujifunza na kuangalia namna ya kendeleza utalii wetu hasa katika kipindi hiki cha kukabiliana na janga Uviko 19 lililoikumba dunia”amesisitiza Mhe. Masanja.
Aidha, Mhe. Mary Masanja ameongeza kuwa ushiriki huo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na pia kuvitangaza vivutio vya Utalii vilivyoko nchini Tanzania ikiwa ni moja ya juhudi za kuunga mkono kazi anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii duniani.
Tanzania huadhimisha Siku ya Utalii Duniani kila mwaka Septemba 27 na kauli mbiu ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka huu ni “Utalii kwa Maendeleo Shirikishi/ Jumuishi