Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo kwa Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
…………………………………………………………………………
Na. Mwandishi Wetu-Moshi
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma nchini kuitekeleza kwa vitendo na weledi kaulimbiu ya KAZI IENDELEE ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inayolenga kuwahimiza kulitumikia taifa kwa kuweka maslahi ya taifa mbele.
Akizungumza na Watumishi wa Umma wa Manispaa ya Moshi, Mhe. Ndejembi amesema, kaulimbiu hiyo inawataka Watumishi wa Umma kuongeza kasi na bidii ya kuchapa kazi ili taifa liweze kunufaika na uwepo wa rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Ameongeza kuwa, ni wajibu wa Watumishi wa Umma kukumbushana umuhimu wa kuendelea kujitoa na kulitumikia taifa kwa weledi mkubwa na kuweka maslahi ya taifa mbele na si maslahi binafsi.
“Kumekuwa na tabia ya baadhi ya Watumishi wa Umma kuweka mazingira ya kujipatia fedha isivyo halali ndio wawahudumie wananchi, kitendo ambacho hakikubaliki katika Utumishi wa umma,” Mhe. Ndejembi amefafanua.
Sanjari na hilo, Mhe. Ndejembi amekemea kitendo cha baadhi ya Watumishi wa Umma kujiona miungu watu ili wanyenyekewe wakati wameajiriwa na Serikali kwa ajili ya kuutumikia umma na si kujikweza.
“Wewe ni Mtumishi wa Umma halafu unataka uogopwe, uogopwe kwa kipi wakati kazi yako ni kuwatumikia wananchi,” Mhe. Ndejembi amesisitiza na kuongeza kuwa ni lazima tuwe wawakilishi bora wa Serikali yetu kwa kuwahudumia wananchi ipasavyo ili Serikali ifikie malengo yake, hivyo
Ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi Mkoani Kilimanjaro imelenga kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa kuzingatia Kaulimbiu ya KAZI IENDELEE kwa maendeleo ya taifa.