Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano ulioandaliwa  kwa pamoja kati ya Tume ya Mipango Sekta binafsi na Asasi za Kiraia kuhusiana na kukuza Ubia na Majadiliano kuhusu mikakati ya kitaifa Kikanda na Kimataifa uliofanyika katika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar.

‘

Mwandishi wa Habari wa Daly News Issa Yussuf akiuliza maswali katika mkutano wa Waandishi wa Habari ulioandaliwa  kwa pamoja kati ya Tume ya Mipango Sekta binafsi na Asasi za Kiraia kuhusiana na kukuza Ubia na Majadiliano kuhusu mikakati ya kitaifa Kikanda na Kimataifa uliofanyika katika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar.

Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Karim  akiuliza maswali katika mkutano wa Waandishi wa Habari ulioandaliwa  kwa pamoja kati ya Tume ya Mipango Sekta binafsi na Asasi za Kiraia kuhusiana na kukuza Ubia na Majadiliano kuhusu mikakati ya kitaifa Kikanda na Kimataifa uliofanyika katika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar.

Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Kitaifa Tume ya Mipango Jamila Abdalla Seif akitoa ufafanuzi baadhi ya maswali yalioulizwa  katika mkutano wa Waandishi wa Habari ulioandaliwa  kwa pamoja kati ya Tume ya Mipango Sekta binafsi na Asasi za Kiraia kuhusiana na kukuza Ubia na Majadiliano kuhusu mikakati ya kitaifa Kikanda na Kimataifa uliofanyika katika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar.

Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa mataifa la mipango ya maendeleo (UNDP)Kimwaga Muhiddin Ali akijibu maswali  katika mkutano wa Waandishi wa Habari ulioandaliwa  kwa pamoja kati ya Tume ya Mipango Sekta binafsi na Asasi za Kiraia kuhusiana na kukuza Ubia na Majadiliano kuhusu mikakati ya kitaifa Kikanda na Kimataifa uliofanyika katika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar.

Mkurugenzi wa Mtendaji ANGOZA  hassan Khamis Juma (katikati)akifafanua jambo wakati akitoa hotuba kwa Waandishi wa Wabari kuhusiana na Mkutano utakao fanyika katika Ukumbi wa Madinatul-bahari utakao zungumzia kuhusu Kukuza Ubia na Majadiliano kuhusiana na mikakati ya Kitaifa ,Kikanda na Kimataifa  uliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.wa mwanzo kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Kitaifa Tume ya Mipango Jamila Abdalla Seif  na kushoto ni Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa mataifa la mipango ya maendeleo (UNDP)Kimwaga Muhiddin Ali.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
………………………………………………………………………………

Na Rahma Khamis Maelezo

Mkutano wa kukuza Ubia na Majadaliano na Utekelezaji wa Mikakati ya kitaifa,kikanda na kimataifa kati ya wadau wa taasisi binafsi na watendaji wa Serikali visiwani Zanzibar unatarajiwa kufanyika kesho Madinatu Albahar Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

                                                                                       

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tume ya Mipango Zanzibar Hassan Yussuf Juma katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo amesema mkutano huo utawashirikisha zaidi ya washiriki 100 kutoka Unguja na Pemba.

Alisema katika mkutano huo wanatarajia kujadili malengo mbalimbali ya kimsingi ambayo yatakuza sekta zote kiuchumi ikiwemo kujadili na kutengeza mikakati ambayo itahakikisha majukumu ya Serikali na wadau wengine katika kutekeleza na kufikia shabaha ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.

 

Malengo mengine ni kukuza ubia uliopo baina ya Serikali na sekta binafsi pamoja asasi za kirai katika utekelezaji wa malengoya maendeleo endelevu Zanzibar.na kupata mapendekezo na shughuli ambazo zitachukuliwa na kufanyiwa kazi na UNDP,ZPC,Sekta binfsi Asasi za kiraia na wadau muhimu wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Zanzibar.

Aidha amesema kuwa katika mkutano huo mada  mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mchango wa Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Zanzibar , Ushiriki wa Sekta binafsi na matokeo ya maendeleo endelevu Zanzibar  pamoja na Mchanganuo  wa Taarifa kijinsia katika ufatiliaji na kuripoti malengo ya maendeleo endelevu Zanzbar.

“Mada ya mwisho itahusiana na Uratibu, Utekelezaji, Ufatiliaji Tathmini ya Mipang ya Maendeleo  Endelevu ya Kitaifa,Kikanda na Kimataifa, ambapo washiriki wa Kongamano hilo watapata fursa ya kuchangia mada zote hizo,”alisema Mkurugenzi huyo.

Nae Mkuu wa kitengo cha Ufatiliaji na Tathmini Tume ya Mipango Jamila Abdallah Seif amesema watu wengi wamekua na uelewa mkubwa na agenda 2030 ambayo utekelezaji wake ulianza Zanzibar tokea mwaka 2019 na kufanyika mikutano katika ngazi ya jamii na waandishi wa habari waliokuwa wakitoa ripoti kwa kila mkutano uliofanyika katika sehemu husika.

Aidha amefahamisha kuwa mkutano huo ulijikita katika kuzungumza juu ya malengo ya maendeleo endelevu Mjini na Vijijini  hivyo wanawashukuru kwa kuwasaidia kukuza uwelewa wa wananchi.

 Mkutano huo unaoandaliwa na kwa pamoja kati ya Tume ya Mipango,Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia ambapo  mgeni rasmi anatarajiwa kua Waziri a nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango  Mh Jamal Kassim Ali na Kaulimbiu ya mwaka huu KUKUZA UBIA WA SERIKALI KITAIFA KIKANDA NA KIMATAIFA KUTAPELEKA  KUFIKIA MALENGO YALIYOKUSUDIWAKWA HARAKA ZAIDI