Ad imageAd image
By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Full Shangwe BlogFull Shangwe Blog
  • Home
  • Biashara
  • Burudani
  • Magazeti
  • Mchanganyiko
  • Michezo
  • Siasa
  • Teknolojia
  • TV
  • Makala
Reading: HOSPITALI YENYE HADHI YA KUWA HOSPITALI YA RUFAA YAFUNGULIWA KIJIJI CHA MARUA -KILIMANJARO
Share
Aa
Aa
Full Shangwe BlogFull Shangwe Blog
Search
  • Home
  • Biashara
  • Burudani
  • Magazeti
  • Mchanganyiko
  • Michezo
  • Siasa
  • Teknolojia
  • TV
  • Makala
Follow US
© 2022 Flavour Media Company Limited. All Rights Reserved. Designed by Yatosha Web Services
Mchanganyiko

HOSPITALI YENYE HADHI YA KUWA HOSPITALI YA RUFAA YAFUNGULIWA KIJIJI CHA MARUA -KILIMANJARO

Alex Sonna
Last updated: 2019/08/08 at 12:03 PM
Alex Sonna 6 years ago
Share
SHARE

Hospitali mpya ya St Monica iliyojengwa na Taasisi ya Kirua Children Care Foundation katika kijiji cha Marua ,kata ya Kirua Vunjo Magharibi katika wilaya ya Moshi.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri Amedeus Macha wakielekea katika ufunguzi rasmi wa Hosptali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitia saini katika kitabu cha wageni alipofika katika Hosptali hiyo kwa ajili ya ufunguzi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri Amedeus Macha akimueleza jambo mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira wakati akitembelea vyumba vya kulaza wagonjwa katika Hosptali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akitizama baadhi ya mashine zilizoko katika Hospitali hiyo.
Chumba cha kulaza wagonjwa.
Padri Amedeus Macha akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira chumba maalumu kwa ajili ya wanawake kujifungulia.
Baadhi ya Vifa vilivyopo maabara ya Hospotli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira  akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitoa kitambaa kufungua jengo hilo la Hosptali ya St Monica.
Padri Amedeus Macha akifanya Ibada mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa Hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya St Monica iliyopo jimbo la Vunjo wilaya ya Moshi.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Mkuu huyo wa mkoa.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica.
Baadhi ya wananchi waliofika katika ufunguzi wa Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri ,Amedeus Macha akizungumza katika ufunguzi wa Hosptli hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Kiliamanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kushuhudia ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica iliyopo kijiji cha Marua ,wilaya ya Moshi .
  Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV .
MBUNGE WA Jimbo la Vunjo ,James Mbatia ameshauri
kuanzishwa kwa Utalii wa Tiba (Medical Tourism) katika eneo linalozunguka
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ili kurahisha utoaji wa huduma
kwa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mbatia aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi rasmi
wa Hospitali ya St Monica iliyopo jirani na Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro katika kijiji cha Marua ,kata ya Kirua Vunjo Magharibi,katika
wilaya ya Moshi  huku akiiomba serikali
kusaidia katika uboreshaji wa Miundombinu ya barabara.
 
Akizungumza
mara baada ya kufungua na  kutembelea
maeneo mbalimbali ya Hospitali Hospitali iliyojengwa na Taasisi ya Kirua
Children Care Foundation Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna
Mghwira ameipongeza taasisi hiyo kwa kujenga Hosptali hiyo ambayo itasaidia
kupunguza changamoto za kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo na mkoa wa Kilimanjaro
kwa ujumla.
.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation
Padri Amedeus Macha amesema Hospitali hiyo itakayo kuwa na uwezo wa vitanda zaidi
ya 100 imelenga kutoa huduma za matibabu kwa wazee na watoto ambao  kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali
mrefu kufuata huduma za Afya.
 
Dkt.Bogias
Mwamgunda ni mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro hapa akaeleza
namna ambavyo Hosptali hiyo itasaidia Wazee na watoto katika kupambana na
magonjwa yatokanayo na Baridi .
 
Taasisi
za Dini katika jimbo la Vunjo zimekuwa mstari wa mbele katika uwekezaji wa
masuala ya huduma za afya ,hali inayochangia urahishaji wa upatikanaji wa
matibabu tofauti na ilivyokuwa kwa kutembea umbali mrefu  hasa nyakati za
mvua na usiku .
 
  
 

 

 
Alex Sonna August 8, 2019 August 8, 2019
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article MHE.AWESO AITAKA HALMASHAURI YA TARIME KUVUNJA MKATABA NA MKANDARASI WA KAMPUNI YA KUMBA QUALITY LTD
Next Article SMZ YAUPONGEZA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE NCHINI

Find Us on Socials

Full Shangwe BlogFull Shangwe Blog

© 2022 Flavour Media Company Limited. All Rights Reserved. Designed by Yatosha Web Services

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

[contact-form-7 id="250336" title="newslatter"]
Zero spam, Unsubscribe at any time.
adbanner
AdBlock Detected
Our site is an advertising supported site. Please whitelist to support our site.
Okay, I'll Whitelist
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?