Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimsikiliza akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa (Bohari ya Dawa) MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo leo Jumanne Agosti 8, 2019 katika maonesho ya 4 ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Conference Centre jijini Dar es salaam katikati ni Marco Masala Meneja Manunuzi ya SADC na Faith Edmin Afisa Manunuzi SADC.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWEBLOG)
………………………………………..
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema moja ya mafanikio makubwa ambayo Tanzania itayapata kama mwanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika SADC ni (Bohari ya Dawa) MSD kufanya manunuzi ya pamoja kwa nchi za SADC.
Mwalimu amesema nchi za SADC zipo tayari kununua dawa kutoka kwa MSD kama msambazaji wao jambo ambalo llitaleta manufaa kwa Tanzania lakini pia litazinufaisha nchi hizo kwa punguzo la bei tofauti na kununua dawa wenyewe kutoka viwandani.
Ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la MSD katika maonesho ya nne ya wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam leo.
Amefafanua nchi za Lethoto, Botswana, Mouritius, Shelisheli na zingine ziko tayari kusambaziwa lakini jambo linallochelewesha ni taratibu za manunuzi ambazo tayari MSD inazifanyia kazi na wakati wowote kazi ya kusambaza dawa katika nchi hizi za SADC itaanza mara baada ya taratibu kukamilika taratibu hizo.
“MSD iko tayari kuwasambazia dawa mpaka kwenye vituo vyao vya afya na hospitali kinachosubiriwa ni kukamilika kwa taratibu za manunuzi ili kazi hiyo ianze kufanyika” Amesema Mwalimu.
Amesema kuwa kwa nchi hizi za SADC kuitumia MSD kama msambazaji wa dawa katika nchi zao itawasaidia sana kwa sababu wataagiza dawa kwa pamoja jambo ambalo litawapunguzia gharama za manunuzi ya dawa.
“Unajua kupatana bei za kununua dawa viwandani ukiwa peke yako ni ngumu kupata punguzo la bei lakini mkiagiza kwa pamoja gharama zitapungua itazisaidia nchi hizi kutoa huduma bora zidi kwa wananchi,”amesema Mwalim .
Pia nasisi Tanzania tutafaidika kama taifa kwa kufanya biashara na wenzetu katika jumuiya na haya ndiyo malengo haswa ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Magufuli.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa (Bohari ya Dawa) MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo leo Jumanne Agosti 6, 2019 katika maonesho ya 4 ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Conference Centre jijini Dar es salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya taifa Muhimbili DKT.Juma Mfinanga wakati alipotembelea banda la MSD wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa (Bohari ya Dawa) MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu na Mkurugenzi Idara ya Afya na Dharura Wizara ya Afya Dk. Elias Kwesi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimsikiliza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya taifa Muhimbili DKT.Juma Mfinanga kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Afya na Dharura Wizara ya Afya Dk. Elias Kwesi na Mkurugenzi Mkuu wa (Bohari ya Dawa) MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiangalia moja ya mashine ya Mfumo wa hewa alipotembelea banda la MSD kushoto ni Etty Kusiliuka Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MSD.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiangalia baadhi ya kliniki maalum za kijeshi zilizotolewa na JWTZ kwa ajili ya utayari wa kuwahudumia washiriki wa maonesho na mkutano wa SADC wanaoweza kuugua ghafla.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimsikiliza Meja Dr. Andrew Israel Lizer wakati alipotembelea kiliniki maalum zilizotolewa na JWTZ kwa ajili ya kuwahudumia washiriki wa Mkutano wa SADC.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipiga picha na wataalam mbalimbali kutoka JWTZ waliopo katika Maonesho na Mkutano wa SADC kwa ajili ya utayari wa kuwahuduimia washiriki wa mkutano huo kwa magonjwa ya dharura.