Pichani kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick (kushoto) wakionesha mmoja kati ya mikataba mitano ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar, tukio hilo limefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Pichani kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick (kushoto), wakisaini mmoja kati ya mikataba mitano ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar, tukio hilo limefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza jambo mara baada ya kusaini mikataba mitano ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar, tukio hilo limefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa fedha na Mipango,Ofisi ya Rais Zanzibar Mhe,Jamal Kassim Ally (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick wakibadilishana mmoja kati ya Mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamanni ya dola za Marekani milioni 292,sawa a shilingi bilioni 674.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi iliyoko katika sekta ya Nishati na kuboresha maisha ya Wananchi wa Zanzibar.Tukio hilo lilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa fedha na Mipango,Ofisi ya Rais Zanzibar Mhe,Jamal Kassim Ally (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick wakionesha mmoja kati ya Mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamanni ya dola za Marekani milioni 292,sawa a shilingi bilioni 674.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi iliyoko katika sekta ya Nishati na kuboresha maisha ya Wananchi wa Zanzibar.Tukio hilo lilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
……………………………………….
Benki ya Dunia nchini na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimetiliana, saini mikataba mitano ya mikopo ya masharti nafuu kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa! (International Development Association – DA) yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.167 (sawa na takribani shilingi trilioni 2.697.
Mikataba hiyo imesainiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Mwigulu Lameck Nchemba kwa upande wa Serikali Tanzania na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Mara Warwick Benki ya Dunia Mikopo nafuu ambayo itasaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania
Miradi hiyo ni (e Tanzania Roads to Inclusion and Socioeconomic Opportunities (RISE) wenye thamani ya dola za Marekani milioni 300 (sawa na takribani shilingi bilioni 693.2); Higher Education for Economic Transfornation (HEET) wenye thamani ya dola za Marekani milioni 425 (sawa na takribani shilingi billioni 982.1); Digital Tanzania Project (DTP) wenye thamani ya dola za Marekani milioni 150 (sawa na takribani shilingi bilioni 346.6); Zanzibar Energy Sector Transformation and Access (ZESTA) wenye thamani ya dola za Marekani milioni 142 (sawa na takribani shilingi bilioni 328.1); na Boosting Inclusive Growth for Zanzibar: Integrated Development (BIG-Z) wenye thamani ya dola za Marekani milioni 150 (sawa na takribani shilingi bilioni 346.6).
Miradi iliyosainiwa inazingatia utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III) na sehemu ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kujenga Uchumi Shindani wa Viwanda kwa Maendeleo ya Wananchi kupitia: uboreshaji wa miundombinu; upatikanaji wa nishati ya kuaminika; kuimarisha mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji; na kuimarisha mifumo ya elimu na mafunzo nchini. Miradi hii mitano (5) inaongeza thamani ya miradi (portfolio) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia hadi kufikia dola za Marekani bilioni 5.5.
Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA) lililoanzishwa mnamo mwaka 1960, limejikita kusaidia nchi masikini zaidi duniani kwa kutoa misaada na mikopo isiyo na riba, kutekeleza miradi inayolenga kuongeza ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini, na kuboresha maisha ya watu masikini.
IDA ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya msaada kwa nchi 76 masikini duniani, kati ya hizo 39 zinatoka Afrika, Rasilimali za IDA huleta mabadiliko chanya kwa watu bilioni 1.6 wanaoishi katika nchi ambazo zinastahili msaada wake. Tangu 1960, IDA imesaidia shughuli za maendeleo katika nchi 113.
Ahadi za IDA za kila mwaka zimefikia wastani wa dola za Marekani bilioni 21 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, na asilimia 61 ya fedha ikielekezwa bara la Afrika.
Kwa viwango vya Benki Kuu vya ubadilishaji wa sarafu kwa tarehe 18 Agosti 2021 vya dola Marekani 1 = shilingi 2,310.85.