Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul wa pilikutoka kulia akiwa na mbunge wajimbo la Iringa mjini Mh. Jesca Mtambasavangu na msanii Mrisho mpoto wakionesha medali zao mara baada ya kushiriki mbio za ASAS Half Marathon 2021 mjini Iringa.
………………………………..
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul ametoa rai kwa uongozi wa wilaya ya Iringa kuhamasisha watumishi wa Umma, Taasisi mbalimbali pamoja na wananchi kushiriki mazoezi ili kuimarisha afya zao hatua itakayowasaidia kufanya shughuli za maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Mhe. Gekul ametoa rai hiyo 07 Agosti, 2021 mjini Iringa wakati alipokuwa Mgeni Rasmi katika mbio za ASAS Half Marathon zilizofanyika mkoani humo.
“Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Iringa, nikuombe uandae utaratibu kwa watumishi kushiriki mazoezi angalau mara tatu kwa wiki ili waweze kuimarisha afya zao ambazo” amesema Mhe. Gekul
Naibu Waziri Gekul ameipongeza Kampuni ya ASAS kwa kuandaa mbio hizo kwa mara ya kwanza na kuatoa rai mbio hizo kuendelezwa na kusisitiza umuhimu wa wadau wengine kuandaa mbio mbalimbali ili kuibua vipaji vya wanamichezo na kuimarisha afya zao.
Mbio hizo zimeshirisha wakimbiaji kutoka katika mikoa mbalimbali nchini, wasanii pamoja na watu mashuhuri ambapo washindi wa kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake kila mmoja amezawadiwa Ng’ombe wa Maziwa mwenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne pamoja na fedha taslimu kwa washindi wa pili na watatu.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akiwa katika picha ya pamoja na msanii Mrisho Mpto wakiwa na medali zao mara baada ya kumalizia mbia=o hizo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akiwa tayari kwa ajili ya kutoa zawadi kwa washindi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akiwa katika picha ya pamoja na washindi mara baada ya kumkabidhi mshindi wa kwanza kilomita 21 kwa wanaume Emmanuel Giniki kutoka Manyara mfano wa picha ya Ng’ombe baada ya kuibuka bingwa wa mbio hizo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akiwa katika picha ya pamoja na washindi mara baada ya kumkabidhi mshindi wa kwanza kilomita 21 kwa wanawake Sara Hiti kutoka Manyara mfano wa picha ya Ng’ombe baada ya kuibuka bingwa wa mbio hizo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akiwa Ng’ombe wawili ambao wamekabidhiwa kwa washindi wa ASAS Half Marathon 2021 kwa washindi wa kwanza kilomita 21 wanaume wanaume na wanawake baada ya kuibuka bingwa wa mbio hizo.
…………………………………………