Na Mwamvua Mwinyi,Mwanabwito
MKAZI wa Kitongoji cha kazi Mwanabwito Kata ya Kikongo Halmashauri ya Kibaha (Kibaha Vijijini) Mkoa wa Pwani Ramadhani amenusurika kuuawa kwa mkuki na wafugaji jamii ya Wasukuma.
Tukio hilo limetokea baada ya mmoja wa wakulima kuwakataza wasiingize mifugo kwenye shamba la jirani yake, ambapo walipokatazwa kabla ya tukio hilo walimjeruhi mkulima kwa kumpiga kwa fimbo kisogoni na mkononi ambapo hali iliyosababisha mkulima huyo kushonwa.
Akizungumza mbele ya Waandishi mkazi huyo alisema kuwa wakulima walikuwa wanane wafugaji sita kabla ya kuitana na kuwa wengi zaidi ambao walimfukuza wakiwa na mikuki, lakini aliwahi kujificha kwenye mabua yanayoota kandokando ya mto Ruvu ndio ikawa salama yake.
“Walinikimbiza umbali zaidi ya kilometa meta na ushehe, wenzangu walikuwa juu ng’ambo ya mto wakiniita simu niliweka mtetemo ili isisikike, nilikaa kwenye mabua hayo kwa zaidi ya dakika saba walipoona kimya wakajua nilishavuka mto, wakageuka na kurejea kuchukua ng’ombe wao,” alisema Pwimwilu.
Mkazi aliyejeruhiwa akijitambulisha kwa jina la Yohana Mrope alisema kuwa aliona makundi ya ng’ombe ikiingia katika shamba la jirani yake alipokwenda kumsaidia alishtukia amepigwa fimbo ya kisogoni na mkononi hali iliyomsababishia ashonwe na kwamba ana RB wanawatafuta waliomshambulia na kuongeza kwamba anawatambua.
Nao wakulima waluojitambulisha kwa majina ya Ashura Asha Kawa na Taison Taison walisema kuwa hali ni mbaya kwani mifugo imekuwa kero kubwa kiasi cha kuwavunja nguvu wakulima, huku wakiiomba serikali iwasaidie kuondokanaa na changamoto hiyo waliyoielezea kuwa ni ya muda mrefu.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Juma Tupa alithibitisha kuwepo kwa kero hiyo, na kwamba wamefika kwenye ofisi zote pasipo mategemeo hivyo tegemeo la pekee kwa Rais Mama Samia Suluhu.
“Hili suala la kero ya mifugo katika Kitongoji changu imekuwa kero kubwa wananchi wangu wanashibdwa kulima kwa kuhofia mifugo, unapolima ujue umejipalilia makaa hautokuwa na muda wa kufanya shughuli yeyote ya maendeleo, kuanzia asubuhi mpaka jioni kazi yako kulinda ng’ombe mpaka unavuna,” alisema Singa