Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Pauline Gekul pamoja na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh. Jesca Msambatavangu wakishiriki mbio za kilomita 5 kwenye mbio za ASAS Half Marathon 2021 zinazofanyika leo mjini Iringa zikianzia kwenye uwanja wa Samora.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Pauline Gekul pamoja na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh. Jesca Msambatavangu wakijiandaa wakishiriki mbio za kilomita 5 kwenye mbio za ASAS Half Marathon 2021 zinazofanyika leo mjini Iringa zikianzia kwenye uwanja wa Samora
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Pauline Gekul akijadiliana jambo na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh. Jesca Msambatavangu kabla ya kushiriki mbio za kilomita 5 kwenye mbio za ASAS Half Marathon 2021 zinazofanyika leo mjini Iringa zikianzia kwenye uwanja wa Samora
Washiriki wa mbio za Kilomita 5 wakianza mbio za kilomita 5 kwenye mbio za ASAS Half Marathon 2021 zinazofanyika leo mjini Iringa zikianzia kwenye uwanja wa Samora
Mabalozi wa ASAS DAIRIES LTD ambao ni wasanii mbalimbali pamoja na watangazaji wakijiandaa kushiriki mbio za kilomita 5 kwenye mbio za ASAS Half Marathon 2021 zinazofanyika leo mjini Iringa zikianzia kwenye uwanja wa Samora
Washiriki wa mbio za ASAS Half Marathon 2021 kilomita 21 zinazofanyika leo mjini Iringa zikianzia kwenye uwanja wa Samora.
………………………………….
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Pauline Gekul ameshiriki mbio za ASAS Half Marathon 2021 zinazofanyika leo mjini Iringa zikianzia kwenye uwanja wa Samora.
Mh. Gekul amezindua na kushiriki mbio hizo pamoja na viongozi wengine wakiwemo wa mkoa wa Iringa na maeneo mengine, wanamichezo na wasanii mbalimbali ambao wamejitokeza kwa wingi ili kushiriki katika mbio za ASAS Half Marathon 2021
Lengo la mbio hizo pamoja na kufanya mazoezi ili kuweka mwili sawa kiafya pia zitachangia vifaa mbalimbali katika sekta ya afya ili kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19 katika hospitali ya wilaya ya Iringa ikiwa ni utaratibu wa Kampuni ya ASAS DAIRIES LTD kujiweka karibu kwa jamii na kuisaidia.
Katika mbio hizo za ASAS Half Marathon 2021 kutakuwa na mbio za Kilomita 21, Kilomita 10 na Kilomita 5 ambapo mshindi wa kwanza kwa wanaume katika umbali wa Kilomita 21 atapata zawadi ya Ng’ombe mmoja ikiwa ni sawa na mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wa wanawake.
Pia kutakuwa na zawadi za fedha taslimu kwa washindi mbalimbali wa kwanza katika umbali wa kilomita 10 na kilomita 5 kwa wanaume na wanawake.